Kurasa

Friday, 31 October 2014

Mastaa wanne Yanga kuikosa Kagera

WACHEZAJI wanne wa kikosi cha Yanga wataikosa mechi ya wikiendi hii dhidi ya Kagera Sugar baada ya kukumbwa na matatizo mbalimbali.
Daktari wa Yanga, Juma Sufiani, amewataja wanne hao kuwa ni mabeki; Nadir Haroub ‘Cannavaro na Kelvin Yondani wanaosumbuliwa na malaria, winga machachari Simon Msuva anayesumbuliwa na mgongo wakati Hussein Javu yeye ameumia goti.
Sufiani alisema kuwa Msuva aliumia mazoezini wakati Javu aliumia goti kwenye mechi dhidi ya Stand United wikiendi iliyopita.
“Wote tumewaandikia mapumziko ya wiki nzima ili waweze kupona kabisa, si matatizo makubwa, lakini ni vyema wakapumzika. Javu atafanyiwa vipimo baada ya kurejea Dar ili kubaini ukubwa wa tatizo lake,” alisema Sufiani.
Katika hatua nyingine, beki wa kulia wa Yanga, Oscar Joshua, ameweka wazi siri ya safu yao ya ulinzi kufanya vizuri akisema ni namna wanavyonolewa na kocha Marcio Maximo.
Alisema: “Ubora wa safu yetu kusema kweli, siri ni kujituma wenyewe, lakini pili ni kufuata maelekezo ya kocha wetu Maximo kwani mfumo anaotufundisha wa namna ya kuzuia, kuijenga ngome yetu lazima ufanye kazi.
“Kocha amekuwa akitupa mbinu ambazo ni ngumu kwa wapinzani kutupita. Kazi hii iliimarishwa mara baada ya mechi ile tuliyofungwa na Mtibwa. Kwa staili hii tunayocheza, hata kama mimi sitakuwepo au mwingine yeyote, atakayeingia akicheza kwa maelekezo, ni ngumu kufungwa,”alisema Oscar.

No comments:

Post a Comment