Kurasa

Saturday, 29 November 2014

KAMATI YA BUNGE YATOA MAPENDEKEZO VIONGOZI HAWA WAFUKUZWE NA WASHTAKIWE...KUTOKANA NA KASHFA YA AKAUNTI YA ESCROW

PRO. MUHONGO
PROF. ANNA TIBAIJUKA
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JAJI WEREMA
MH.WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

HALI YA SASA YA VVU/UKIMWI


Print

Hali ya UKIMWI Nchini

Utafiri wa kiashirio cha VVU/UKIMWI na malaria Tanzania 2011-2012 umejumuisha kwa
 kupima zaidi ya wanawake na wanaume20,811. Kwa mujibu wa utafiti huo asilimia 5.1 ya
 watanzania wenye umri wa miaka  15-49 wanamaambukizo ya VVU/UKIMWI. 

Maambukizo ya VVU/UKIMWI ni ya kiwango cha juu miongoni mwa wanawake kuliko
 wanaume katika maeneo ya mijini na vijijini. Wakazi wa mijini ni mara mbili zaidi ya
 wakazi wa vijijini. 

Maambukizo ya VVU/UKIMWI Tanzania yamepungua katika miaka ya hivi karibuni. 
Kiwango cha hivi karibuni cha maambukizo ya VVU/UKIMWI ni 5.1% ambapo 6.2% 
ni wanawake na 3.8.% ni wanaume. Kwa kulinganisha na utafiti wa kiashirio cha
 VVU/UKIMWI Tanzania mwaka 2007-2008 (THIS) umebaini  maambukizo ya jumla 
ya VVU/UKIMWI kuwa ni 5.7%, 

Maambukizo ya VVU/UKIMWI ni ya juu zaidi katika mkoa wa Njombe (14.8%), 
Kiwango cha maambukizo ni cha chini zaidi Pemba ambayo ni chini ya (1%). 

Kwa wanawake na wanaume viwango vya maambukizo ni vya juu zaidi miongoni mwa
 wajane au walio talikiwa (walioachwa) kuliko wajane au wasio oa au kuolewa au walio oana 
hivi karibuni. Kati ya wanawake wajane wanne, mmoja ana virusi.


Visababishi vya VVU/UKIMWI
Mwenendo na vibainishi vya janga la UKIMWI nchini ni vingi na vinaongozwa na
 uhusiano wa kingono wa watu wa vipengele vingi vya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi.
 Kwa ujumla, vibainishi vya janga la UKIMWI nchini huenda visitofautiane sana na
 vile vya sehemu nyingine za Afrika zenye maambukizo ya UKIMWI 

yaliyoenea nchi nzima. Miongoni mwa vipengele muhimu ni pamoja na vifuatavyo:

v  Uasherati
v  Matumizi madogo na yasiyo endelevu ya kondomu
v  Ngono za marika yanayotofautiana sana
v  Kuwa na wapenzi wengi.
v  Ukosefu wa elimu ya maambukizo ya UKIMWI
v  Kuwepo kwa maradhi mengi ya ngono kama vile tutuko, homa,

v  Jando kwa wanaume
Sababu za mahali husika, za kushamiri kwa janga nchini ni:

Ø  Umaskini na biashara ya ngono pamoja na ongezeko la wafanyabiashara 
   wa ngono
Ø  Tabia mbaya za ngono za wanaume kutokana na kuruhusiwa kimila kuwa
    na nguvu
Ø  Kukosekana usawa wa kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijinsia pamoja na
   unyanyaswaji wa wanawake na wasichana walio ndani na nje ya mahusiano.
Ø  Matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
Ø  Tabia za kimila (kama vile utakasaji wajane na jando na unyago)
Ø  Safari za aina zote zinazosababisha kuwa mbali kwa wanandoa 
   na ongezeko la mahawara

Ø  Kutokutahiriwa