WIKIENDI iliyopita katika Uwanja wa
Sokoine jijini hapa kulikuwepo na mechi mbili za Ligi Kuu Bara kati ya Simba na
Prisons iliyochezwa Jumamosi, Mbeya City na Mtibwa Sugar iliyochezwa juzi
Jumapili.
Mechi zote mbili zilikuwa na
mashabiki wa kutosha huku Simba ikijaza zaidi mashabiki wake kutoka Dar es
Salaam wakati Mbeya City ikiwa na mashabiki wake wazawa, uwingi wa mashabiki
hao ulikuwa na lengo moja tu kuzisapoti timu zao ili zipate ushindi.
Katika mchezo wa Simba na Prisons
matokeo yalikuwa ni sare ya bao 1-1, bao la Simba likifungwa na Emmanuel Okwi
wakati Prisons walisawazisha kupitia mshambuliaji wao Hamis Maingo katika
dakika za lala salama.
Kwa matokeo hayo Simba iliambulia
pointi moja na kufikisha pointi tano katika michezomitano walizocheza dhidi ya
Coastal Union, Stand United, Polisi Moro na Yanga ambazo zote walitoka sare.
Kwa sasa Simba inajiandaa na mechi
yake nyingine ambayo pia watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani
Morogoro ambapo watacheza na Mtibwa Sugar wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 13
wakati Simba wanashika nafasi ya 10.
Mbeya City inashika nafasi ya 11
ikiwa na pointi tano sawa na Simba ingawa wametofautiana kwa mabao ya kufunga
na kufungwa wakati Prisons ina pointi tano na inashika nafasi ya tisa.
Mbeya City inaondoka kesho Jumatano
kuelekea Shinyanga ambako itacheza mechi yake dhidi ya Stand United na baada ya
hapo itasafiri mpaka Bukoba kucheza na Kagera Sugar.
Katika mechi zilichezwa jijini Mbeya
baadhi ya mambo yalionekana kuchangia kupata matokeo mabaya kwa timu hizo mbili
za Simba na Mbeya City ambayo Mwanaspoti imeyafanyia uchunguzi.
Dakika 45 za Simba kipindi
cha pili
Kwa upande wa Simba, Kocha Mkuu
Patrick Phiri alifanya mabadiiko kipindi cha pili kwa kuimtoa Said Ndemla na kumwingiza
Amri Kiemba, alitolewa Ramadhani Singano akaingia Haroun Chanongo. Lakini
kipindi cha kwanza timu hiyo ilicheza vizuri na kupata bao la mapema.
Baada ya mabadiliko hayo, Simba
ilipwaya katikati na kupokea mashambulizi mengi kutoka kwa Prisons ambao
walisawazisha katika dakika za lala salama huku wachezaji wa Simba wakionekana
kuishiwa pumzi na kutokuwa na kasi ya kukimbia na kuwakaba wapinzani wao. Phiri
alikiri kuwa mabadiliko aliyoyafanya yaliigharimu timu yao.
No comments:
Post a Comment