Kurasa

Friday, 14 November 2014

HIFADHI YA AMANI KATIKA MILIMA YA USAMBARA


Kutokana na ongezeko la watu duniani ambalo ni tishio kubwa sana inayoweza kuathiri mazingira yetu, si rahisi kuona tena eneo la mazingira asiliya ambalo halijaguswa na binadamu. Sisi sote, mbali na uraia au asili yetu, tumefikwa na changamoto kubwa sana kwa sababu nafasi ya kuishi katika mazingira safi yenye utajiri kiasiliya inazidi kupungua kila siku. Sisi sote tunataka kukaa katika nyumba nzuri, kupata umeme na maji, kuendesha gari na kupanda ndege, kustawisha mimea na kuchuma mazao mengi kushinda mahitaji yetu, na hali kadhalika. Wakati wa kupendelea hivyo, tuna kawaida ya kujiangalia tu kiubinafsi huku tukipuuza viumbe wanaoishi katika mazingira yetu kwa kufikiri kuwa hawana faida. Hilo ni janga kubwa sana ambalo linatukabili sasa kwa sababu mara nyingi tunakosa elimu ya kutosha.

Kwa bahati nzuri, Tanzania bado ina sehemu asiliya ambazo zinaelekea kuwa hifadhi nzuri, lakini tukizingatia hali jinsi ilivyo kwa mtizamo wa juu juu tu. Hususan hifadhi ya Amani, katika safu ya milima ya Usambara ni miongoni mwa misitu ya asili ambayo serikali ya Tanzania imeamua kuitilia maanani kwa sababu ya thamani baioanuai yake kubwa. La kusisitiza kwanza ni kwamba eneo hilo, pamoja na kwamba lina sehemu nyingi za mazingira asiliiya, vile vile lina watu wengi ambao huishi huku tangu zamani. Si la kushangaza basi, hasa katika muktadha hii, kuona kwamba sura ya milima yake ina vipande vipande vya mashamba ya mchai, ambavyo ni tange zinazomilkiwa na watu, pamoja na miti mingine ya kuleta mapato kwa wakaazi wake. Ina maana kwamba maeneo makubwa sana ya asiliya tayari yameshapotea kusudi binadamu aweze kuchuma mazao yake ya kilimo (hasa mchai, mkarafuu, muwa, mdalasini, mahindi na kadhalika). Siyo kwamba wakaazi hawana haki ya kushughulikia shughuli zao za asili (kulima, kukata kuni, kuchuma miti ya porini, na kadhalika), ila msomaji aelewe kwamba binadamu akizidi kukiuka mipaka ya majukumu yake, yaani akizidi kutumia ardhi anakoishi kupita kiasi, athari juu ya mazingira kwa jumla itakuja kuwa ya kiangamizi.

Kwa kifupi, changamoto kwa siku hizi ni hilo : kutunza mali ya watu bila ya kuangamiza yaliyobaki katika mazingira asiliya. Na kutokana na hali hiyo ya utele, utele wa watu, utele wa nyumba, utele wa gari na kadhalika, imekuwa kama kwamba dunia imekuwa finyu zaidi kila kukicha, kiasi cha kukatisha tamaa ya wataalamu ambao wanajitahidi, kila siku, kuwaelimisha watu ili watunze mazingira yao. Kinachobidi sasa ni kujipatia muamuzi mwafaka ambao itakuwa aina ya suluhisho endelevu kwa watu ambao wamebahatika (ingawa hawajajua kwamba ni bahati) kuishi katika mazingira asiliya mithili ya milima ya Usambara. Watu wana haki ya kuzalisha mazao yao ya kilimo lakini pia wanapaswa kukiri kwamba wanyama wadogo kama vile spishi fulani ya ndege au reptilia ambao ni waendemiki wa Usambara wanastahili kuishi na kuwepo kwa enzi zijazo. Je kweli hilo litawezekana wakati tunaambiwa kwamba asilimia 50 ya misitu imeshapotea ?

Wanyama wa msitu

Wanyama wengi huishi katika milima ya Usambara. Katika jamii ya mamalia, eneo la Amani limesharekodi aina 60 ya spishi mbali mbali, kuanzia panya mdogo hadi nguruwe msitu. Mtembezi huenda atakutana na « nyani wa njano » (kg. yellow baboon, kl. Papio cinocephalus), ni rahisi kumkuta kutokana na tabia yake pole sana. Pamoja na nyani huyo, wanyama wengine wanaoonekana kwa wingi ni kama : mbega (kg. Angola pied colobus, kl. Colobus angolensis), kima bluu (kg. Blue monkey, kl. Cercopithecus mitis), nende mwenye miguu mekundu (kg. Zanj sun squirrel, kl. Heliosciurus undulatus), nende wa milimani (kg. Tanganyika mountain squirrel, kl.Paraxerus lucifer), nende wa pwani (kg. red-bellied coast squirrel, kl. Paraxerus palliatus) nende anayepaa (kg. Lord Derby’s Anomalure, kl. Anomalurus derbianus), koni (kg. black and rufous elephant shrew, kl.Rhynchocyon petersi), kuhe (kg. giant pouched rat, kl. Cricetomys gambianus), komba wa Usambara (kg. Usambara galago, kl. Galagoides species)

Ndege adimu

Ndege katika hifadhi ya Amani wako wengi. Wengi hupatikana katika sehemu mbali mbali za Afrika pamoja na nchi nyingine. Wengine ni adimu sana ama wamezoeleka sana kuishi katika milima hii tu. Ina maana kwamba wanapatikana hapa hapa tu duniani, yaani ni ndege au wanyama andemiki. Wengine wameadimika sana kiasi cha kukumbwa na hatari kubwa ya kupotea kabisa. Mmojawapo ni aina ya ndege mwenye mdomo mrefu anayeitwa « kolokolo domo-refu » (kg. Long-billed forest warbler, kl. Artisornis moreaui ) ambaye yupo katika milima ya Usambara ikiwa ni pamoja na sehemu ndogo ya Msumbiji. Kwa hivyo tunapaswa kuwa makini sana katika kuhifadhi mazingira yake endapo tunataka ndege huyo aonekane tena kwa vizazi vijavyo.

Katika takriban aina 350 ya ndege ambao wamerekodiwa katika milima ya Usambara, 12 wako kwenye takwimu ya ndege walioko katika hatari ya kutoweka duniani. Miongoni mwao wapo « bundi wa sokoke » (kg. Sokoke scops-owl, kl. Otus ireneae), « bundi wa Usambara » (kg. Nduk eagle-owl, kl. Bubo vosseleri), « nofi wa Tanzania » (kg. Nicoll’s weaver, kl. Ploceus nicolli), « chozi milia ya kijani », banded green sunbird (kl. Anthhreptes rubritorques), « chozi Amani » (kg. Amani sunbird ; kl. Anthreptes pallidigaster).

Reptilia na viumbe wengine :

Milima ya Usambara imejaaliwa kuwa na karibu jamii 30 za reptilia, wakiwepo vinyonga, nyoka, kenge na mijusi. Takriban jamii 16 za reptilia hazipatikani mahali pengine popote duniani. Miongoni mwao, ndio vinyonga wanaoonekana kwa urahisi sana, hasa usiku. Wako aina mbali mbali, wenye au wasio na pembe, wadogo kwa wakubwa kiasi.


Amphibia kama chura wapo wengi pia. Amphibia hawapungui chini ya spishi 40. Wengi katika hawa ni waendemiki wa milima ya Usambara wala hawapatikani kwingine duniani. Miongoni mwa chura, wasayansi wana kawaida ya kuainisha kila spishi kufuatana na etolojia yake. Hususan chura wa maji (aina ya Xenopus) huishi ndani ya maji tu wala anashindwa kutoka nje. Tofauti na wengine (jamii ya hyperoliidae) ambao huishi juu kileleni kwa miti.

Mwisho katika viumbe hawa wa kiajabu ni vipepeo. Wako wengi sana na mtembezi hawezi kuwakosa katika matembezi yake. Msomaji anaweza kuangalia tovuti hii ifuatayo kuhusu vipepeo wa Tanzania ambao takriban 130 wanapatikana Tanzania pekee wala hawapo nchi nyingine duniani.

Mimea

Zaidi ya aina 3000 za mimea zimeshatambuliwa kwenye milima ya Usambara. Kiasi kinachokadiriwa kuwa asilimia 25 hadi 30 za aina hizi za mimea zinazopatikana katika safu ya milima ya ukanda wa Mashariki, hazipatikani mahali popote duniani. Kati ya hizi nyinginezo zinapatikana Usambara mashariki tu.

Kwa wingi huo wa aina za mimea katika Afrika, mingi yake ikiwa inapatikana hapa tu, Usambara imepewa sifa ya kuwa sehemu mojawapo duniani yenye sifa za pekee iliyorithiwa kutoka kwa vizazi vilivyopita. Ni dhima kubwa ya hifadhi ya Amani kuhifadhi bioanuai hii ya mimea mingi, miongoni mwao ni mingi ya kiajabu au ya kienyeji kama vile :

Mvule (Milicha exelsa) ni aina muhimu sana ya miti inayotumika katika viwanda vya samani. Mivule mingi inaonekana katika mashamba ya chai.

Kihambie (Drypetes usambarica) ni mti wa ajabu inayo maua na matunda yanayokua kwenye shina la mti.

Mhesi (Maesopsis eminii), ni mti ambao umeenea sana katika eneo la Amani ambao matunda yake huliwa na hondohondo. Ndege huyu hutawanya mbegu zake katika msitu ya Amani na kwingineko.

Mkuti (Chrysophyllum perpulchrum) ni mti ambao hutoa matunda yake kuanzia mwezi wa tano (mei) hadi mwezi wa nane (agosti). Majani yake ni mekundu na matunda yana rangi ya kahawia. Matunda yanapendwa na kima na mbegu zake zinaliwa na mpugi wakati zinapodondoka chini.

Mkuyu msitu (Ficus) nao umeenea pia. Huo mti una tabia ya kuota mizizi yake mikubwa sana na hupenda hali ya unyevu kwenye miamba ambayo dughulishi huota juu yake.

Dughulishi (Saintpaulia magungensis) ni aina ya mmea mdogo wenye maua mazuri sana. Hupenda sana mazingira ya msitu wa Amani.

Mzikoziko (Isolona heinsenii) nao hupatikana lakini kwa nadra sana. Upo katika jamii ya mti maarufu sana ambao ni topetope (au mstafeli, Annonaceae). Ni mti ulioadimika sana katika milima ya Usambara. Wenyeji humtumia kwa kujengea.

Mbewe (Tabernae montana) ni aina ya mti mdogo unaopatikana kwa wingi katika eneo la Amani. Majani yake ni makubwa na matunda ya kahawia ni makubwa kama nazi. Imethibitishwa kwamba matunda yake yanatumika kutibu matatizo ya moyo na figo yanapochanganywa na mimea ya aina nyingine.

Miti mingi mengine ambao ni muhimu ipo kama vile msambo (Allanblackia stuhimannii) ambao mbegu zake huwapatia weneyji mafuta ya kupikia. Mpumu (Anthocleista grandiflora) nao ni mti maarufu pia kwa kuwa na majani mapana sana. Unajulikana kwa kupatikana kwa dawa ya pumu (asthma). Long’we (Cyathea manniana)ni mti pia ambao magome yake hutibu matatizo ya tumbo. Ng’oko (Piper capense) unaota mzizi ambao unatumika katika kujenga nguvu za kiume. Ng’waka (Annickia kummeriae) pia huota magome ambayo huchangia katika kutibu malaria na vidonda.

Kama unataka kuchunguza na kujua zaidi, hii ifuatayo ni tovuti nzuri sana :



MAJI NA JUISI YA LIMAU ASUBUHI KINGA KUBWA MWILINI

MAJI NA JUISI YA LIMAU ASUBUHI KINGA KUBWA MWILINI

TUMEZOEA kuanza siku kwa kunywa vinywaji moto kama vile kahawa au chai na hii imekuwa ndiyo desturi ya maisha ya watu wengi duniani. Lakini siyo lazima kuanza siku yako kwa kunywa vinywaji hivyo, ambavyo tafiti nyingi zimeonesha chai na kahawa vikitumiwa kupita kiasi vinaweza kuwa na athari kwa mtumiaji.
Katika kuangalia njia mbadala na bora ya kufungua kinywa na kuanza siku vizuri, imebainika kuwa glasi moja ya maji ya  uvuguvugu yaliyochanganywa na juisi ya limau kipande kimoja, yana faida kubwa mwilini na yanafaa kutumiwa kama kifungua kinywa asubuhi.
Zifuatazo ni baadhi ya faida kubwa za kunywa maji kwa kuchanganya na juisi ya limau asilia kama zilivyoanishwa na kuthibitishwa na tafiti mbalimbali za kisayansi:

HUSAIDIA USAGAJI CHAKULA: Maji ya uvuguvugu husaidia kuuamsha  na kuuchangamsha utumbo na maji ya limau hulainisha na kuondoa sumu yoyote inayoweza kuwa imeganda kwenye utumbo na kuipeleka kweye njia ya haja kubwa ili kutolewa kama uchafu.
HUONDOA SUMU KWENYE NGOZI NA MWILINI: Unywaji wa maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na juisi ya limau husaidia sana kuondoa sumu na uchafu kwenye ngozi kwa njia ya mkojo. Aidha, kiwango kingi cha Vitamin C kilichomo kwenye juisi ya limau huondoa takataka zote za kwenye mwili na damu, hivyo kuiacha ngozi yako safi, laini na nyororo.
HUIMARISHA KINGA YA MWILI: Kama tulivyoona hapo juu, limau lina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo ni muhimu katika kujenga kinga ya mwili na huzuia magonjwa ya mafua na kikohozi. Halikadhalika limau lina kiwango kingi cha ‘potasiamu’ ambayo huamsha ubongo na kudhibiti shinikizo la damu.
HUONDOA ULEVI WA KAHAWA: Kuna watu wameshazoea kunywa kahawa kila siku na kuwa kama ulevi, kwani wanapokosa kunywa huwa kama wagonjwa, lakini kwa kunywa maji na limau hali hiyo ya ‘uteja’ huondoka na kujisikia huru na mchangamfu.
HUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO: Limau pia lina kiwango kingi cha kirutubisho aina ya kamba lishe (pectin fiber) ambacho ukikila kinakufanya ujisikie kushiba. Hivyo maji haya ni mazuri sana kwa watu wenye kuhitaji kupunguza uzito au kuimarisha uzito walionao.
MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA

Hakikisha kiwango cha joto cha maji utakayotumia kiwe cha kati, si ya moto wala baridi. Maji moto sana siyo mazuri kwasababu yataua virutubisho vilivyomo kwenye limau na ya baridi sana yanaweza kusumbua tumboni. Pia yawe maji safi na salama.
Ili kuyalinda meno yako dhidi ya uchachu wa limau, pendelea kutumia mrija kunyonyea maji hayo. Hakikisha unakamua juisi yako kutoka kipande cha limau halisi na siyo juisi ya limau iliyosindikwa kwenye chupa. 
Ukiwa na mazoea ya kuanza siku yako kwa kunywa mchanganyiko huu wa maji na juisi ya limau, afya yako itaimarika, hutapatwa na magonjwa kirahisi na ngozi yako itakuwa laini na nyororo.

MIMBA KUTOKA (ABORTION)



Tatizo la mimba kutoka au kutolewa ni jambo ambalo limewakumba kina mama wengi walio katika umri wa kuzaa. Aidha mijadala kuhusu kuhalalishwa au kuendelea kuharamishwa kwa utoaji mimba ni jambo linalochukua nafasi ya mazungumzo ya kila siku katika maisha yetu.

Kwa baadhi ya nchi, suala la utoaji mimba ni jambo lililohalallshwa kisheria ingawa kwa nchi kama Tanzania, suala hili halijahalalishwa isipokuwa tu pale panapokuwa na sababu za kitabibu zinazolazimisha kufanya hivyo.

Nini maana ya mimba kutoka (abortion)
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), utokaji mimba (abortion) hutokea pale ambapo kiumbe (mimba) kilicho chini ya wiki 22 kinapotoka kwa sababu moja ama nyingine, au kinapotolewa kwa njia yeyote ile. Aidha shirika la Afya limekwenda mbali zaidi na kutoa maana nyingine ya utokaji mimba kuwa ni pale mtoto (kiumbe) anapozaliwa akiwa na uzito wa chini ya gram 500.

Aidha baadhi ya matabibu hupendelea kutumia neno 'abortion' kumaanisha kitendo cha utoaji wa mimba kinachofanywa na mtu mwingine ama kwa njia sahihi au zisizo sahihi na 'miscarriage' kumaanisha kitendo cha mimba kutoka yenyewe kwa sababu nyingine yeyote. Ukiacha tofauti hizi za jinsi ya kuharibika kwa mimba, abortion na miscarriage humanisha kitu kilekile cha mimba kutoka.

Aina za utokaji/utoaji mimba (Classification of abortion)
Utokaji mimba umeanishwa katika aina zifuatazo
  1. Utokaji wa mimba wa hiyari yaani kitendo cha mimba kutoka yenyewe (spontaneous abortion)
  2. Mimba inayotishia kutoka ingawa bado haijatoka (threatened abortion)
  3. Utokaji wa mimba usioepukika (inevitable abortion)
  4. Utokaji wa mimba ulio kamili (complete abortion)
  5. Utokaji wa mimba usio kamili (incomplete abortion)
  6. Mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
  7. Utokaji wa mimba unaojirudia rudia (recurrent abortion)
  8. Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)
  9. Utoaji mimba kwa sababu za kiafya (therapeutic abortion)

1. Utokaji mimba kwa hiari au kitendo cha mimba kutoka yenyewe (spontaneous abortion)

Hii ni hali inayotokea pale mimba inapoharibika na kutoka bila kuwepo kwa sababu yeyote iliyo dhahiri, kwa maana nyingine mimba uharibika na kujitokea bila kusababishwa na mtu wala kitu chochote.
Utokaji mimba wa namna hii umegawanyika katika aina kuu nne ambazo ni
1.   Mimba inayotishia kutoka ingawa bado haijatoka (threatened abortion)
2.   Mimba isiyoepukika kutoka (Inevitable abortion)
3.   Mimba inayotoka yote au kamili (complete abortion), na
4.   Utokaji mimba usio kamili (Incomplete abortion)

Mimba inayotishia kutoka (threatened Abortion)
Tatizo hili hutokea mapema wakati wa ujauzito. Hali hii hujionesha kwa damu kutoka ukeni wakati njia ya shingo ya uzazi ikiwa bado imefunga. Mara nyingi mimba inayotishia kutoka haina tabia ya kuambatana na maumivu yeyote ya tumbo.

Daktari anapompima mgonjwa hukuta shingo ya kizazi ikiwa imefunga na hakuna dalili zozote za kiumbe kutoka ingawa mgonjwa hutokwa na damu sehemu za siri. Aidha mgonjwa huwa hana maumivu yeyote ya tumbo.
Mimba isiyoepukika kutoka (inevitable abortion)
Hii ni hali inayotokea mapema wakati wa ujauzito pale damu inapotoka ukeni wakati njia ya shingo ya kizazi ikiwa imefunguka au kuwa wazi. Aidha, kwa kawaida, kiasi cha damu kinachotoka ni kingi na mgonjwa hujisikia maumivu makali sana ya tumbo.
Utokaji mimba usioepukika waweza kupelekea

·       Utokaji mimba ulio kamili (complete abortion), au
·       Utokaji mimba usio kamili (incomplete abortion).
·       Utokaji mimba usio kamili (incomplete abortion)
·       Utokaji mimba usio kamili huambatana na utokaji damu kwa wingi

sehemu za siri za mgonjwa, kufunguka kwa njia ya shingo ya kizazi, kutoka kwa baadhi ya mabaki ya kiumbe (products of conception) ingawa mengine hubakia, na mgonjwa kujisikia maumivu makali ya tumbo hususani sehemu za chini ya kitovu.

Utokaji wa mimba ulio kamili (complete abortion)
Hali hii huambatana na mama kutokwa damu sehemu za siri, kujisikia maumivu makali ya tumbo pamoja na kutoka kwa kiumbe ikiambatana na kondo lake la nyuma. Aidha baada ya muda, mgonjwa hueleza kupotea kwa maumivu ya tumbo, damu kupungua kutoka sehemu za siri na kufunga kwa njia ya njia ya shingo ya kizazi (cervix).

Mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
Hali hii hutokea pale ambapo, kiumbe kinapokuwa kimekufa bila ya mimba kutoka. Mara nyingi, damu huwa haitoki sehemu za siri, na mgonjwa huwa hajisikii maumivu yeyote ya tumbo. Aidha huwa hakuna dalili zozote za ukuaji wa mimba na hata mapigo ya moyo ya mtoto hayawezi kutambulika hata kama vipimo maalum vitatumika. 

Utokaji wa mimba unaojirudia rudia (recurrent abortion)
Hali hii hutokea pale ambapo mama huwa na historia ya mimba kutoka mara tatu au zaidi kwa mfululizo.
Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)
Utoaji mimba kinyume cha sheria ni usitishwaji wa maisha ya mimba au kutolewa kwa kiumbe kinyume na sheria za nchi husika zinavyoagiza. Katika mazingira kama haya, sababu dhahiri za kitaalamu hukosekana isipokuwa wahusika hutenda kulingana na sababu zao binafsi zikiwemo za kutoitaka mimba au kama ni muhusika ni mwanafunzi huogopa kufukuzwa shule.

Utoaji mimba kisheria kwa sababu za kitabibu (therapeutic abortion)
Utoaji mimba ulioidhinishwa kitabibu ni usitishwaji wa mimba kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama. Usitishwaji huu ni hufanywa kitaalamu na daktari. Sababu zinazoweza kufanya mimba ikasitishwa ni pamoja na

·       iwapo kiumbe kina mapungufu mengi ya kimaumbile (fetal anomally) ambayo yatamletea mtoto atakayezaliwa matatizo na hata kusababisha kifo chake
·       iwapo mama mjamzito alipata ujauzito kwa kubakwa na asingependa kuzaa, au
·       iwapo mama mjamzito ana kansa , kwa mfano, kansa ya kiwanda cha mayai ya kike (ovarian cancer), kansa ya damu (leukemia) au kansa ya tezi la goita (thyroid cancer)
·       Mambo gani hufanya mimba kutoka kwa hiyari?
·       Kuna sababu kadhaa zinazoweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyari (spontaneous abortion). Miongoni mwa sababu hizo ni
·       Matatizo kwenye mfumo wa jenetiki (genetic abnormalities) ambayo husababisha kuharibika na kutoka kwa mimba katika miezi mitatu ya mwanzoni.
·       Matatizo kwenye mfuko wa uzazi (uterine problems): matatizo kama vile kuwepo kwa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke (uterine fibroids), au kulegea kwa milango ya shingo ya kizazi (cervical incompetence)husababisha mimba kutoka katika theluthi ya pili ya ujauzito (second trimester).
·       Sababu nyingine ni pamoja na maradhi wakati wa ujauzito kama malaria, kisukari, shinikizo la damu, kifafa cha mimba, matatizo kwenye tezi ya 'goita' (hypothyroidism). Aidha maambukizi kama Rubella, toxoplasmosis na mengineyo nayo pia huweza kusababisha mimba kutoka.
·       Kukosekana kwa ulinganifu katika baadhi ya homoni mwilini (hormonal imbalance)
·       Matumizi ya baadhi madawa kwa mfano zinazotumika katika kutibu msongo wa mawazo kama vile paroxetine auvenlafaxine nayo yaweza kusababisha utokaji wa mimba.
·       Tabia hatarishi zinazoweza kusababisha utokaji wa mimba
·       Unywaji pombe uliopitiliza.
·       Uvutaji sigara
·       Utumiaji madawa ya kulevya kama vile kokeini (cocaine)
·       Utumiaji kwa wingi wa vinywaji vyenye kiasili cha caffeine kama vile kahawa au kakao.
·       Vipimo na Uchunguzi
·       Ili kutambua kuwepo kwa hali hii ya mimba kutoka, vipimo vifuatavyo vyaweza kufanywa na tabibu
·       Kipimo cha mimba kwa kutumia mkojo (Urine for hCG)
·       Kupima damu ili kufahamu kiasi cha wingi wa damu (haemoglobin level), kundi la damu (blood group) na muda wa damu kuganda (bleeding and clotting time).
·       Kuchunguza iwapo shingo ya uzazi imefunga au ipo wazi, na pia kuchunguza iwapo kuna dalili ya kiumbe kutoka ama la. Uchunguzi huu huitwa speculum examination.
·       Ultrasound ya nyonga (pelvic utrasound) kwa ajili ya kutambua iwapo kiumbe kipo ama la, na kama kipo je ki hai ama kimekufa.
·       Aidha ni muhimu pia kufanya uchunguzi wa magonjwa mbali ya zinaa ambayo husababisha mimba kutoka.

Matibabu ya utokaji wa mimba
Matibabu ya utokaji wa mimba hutegea sana aina ya utokaji wa mimba. Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia vitu vifuatavyo wakati wa kutoa matibabu kwa mtu aliyepoteza mimba
Wahudumu wa afya huzingatia kanuni zote (ABC) za kuokoa maisha ya mgonjwa kama vile
·         kuhakikisha njia ya hewa ya mgonjwa ipo wazi na hewa inaingia na kutoka vizuri kwenye mapafu
·         kuhakikisha mgonjwa anapumua vizuri bila shida
·         kuhakikisha mishipa ya damu ya mgonjwa imewekwa mrija wa veni (intravenous line) na mgonjwa anapewa dripu ya maji ya normal saline.
·         kuhakikisha mgonjwa anaongezwa damu haraka iwapo vipimo vitaonesha kuwa alipoteza damu kwa wingi
Matibabu ya mimba inayotishia kutoka (threatened abortion)
Kwenye hali hii, mgonjwa hutakiwa             
·         kupumzika kitandani bila kufanya kazi yeyote (complete bed rest) angalau kwa wiki moja au zaidi mpaka hapo damu itakapoacha kabisa kutoka
·         kumpa ushauri na uhakika mama ili kumfanya atulie kiakili (assurance and proper councelling)
·         Mama pia hupewa dawa za kumtuliza na kumfanya apumzike (sedatives) kama vile phernobabitone
·         Aidha mama hupewa dawa kwa ajili ya kupunguza kusukuma kwa uterus (antispamodics) kama vile salbutamol
·         Kutofanya tendo la ndoa kwa wiki mbili au tatu
·         Aidha mama na mumewe hupewa ushauri juu ya tatizo hilo na jinsi ya kuendelea na matibabu
Matibabu ya mimba iliyotoka kamili (complete abortion)

Mara nyingi mgonjwa huwa haitaji matibabu zaidi ya uangalizi wa karibu kwa vile kiumbe pamoja na kondo lake la nyuma vyote huwa vimetoka kikamilifu. Mara chache sana, kulingana na jinsi daktari atakavyoona, mgonjwa anaweza kupewa antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi.

Matibabu ya utokaji wa mimba usiokuwa kamili (incomplete abortion)
Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba uhitaji mgonjwa kusafishwa kwa ajili ya kuondoa mabaki ya kiumbe (products of conception) yaliyobakia. Usafishaji huu huweza kufanywa kwa kutumia njia inayoitwa Manual Vacuum Aspiration (MVA).

Aidha mgonjwa hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa maambukizi ya vimelea vya bakteria. Matibabu mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)

Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba ni pamoja na mgonjwa kuwekewa maji ya uchungu ili kiumbe kiweze kutoka. Wakati mwingine, daktari anaweza kuamua kusafisha mfuko wa uzazi (uterus) kwa kutumia njia inayoitwa dilatation and curettage. Sambamba na matibabu hayo, mgonjwa pia hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vimelea vya bakteria.

Matibabu ya tatizo la utokaji wa mimba unaojirudia (recurrent abortion)
Jambo la msingi katika matibabu ya tatizo la utokaji mimba unaojirudia (recurrent abortion) ni kugundua na kutambua chanzo kinachosababisha tatizo hilo na kisha kukishughulikia ili kuondoa kabisa kujirudia rudia kwa tatizo hili.

·    Kuchunguza iwapo shingo ya uzazi imefunga au ipo wazi, na pia kuchunguza iwapo kuna dalili ya kiumbe kutoka ama la. Uchunguzi huu huitwa speculum examination.

·   Ultrasound ya nyonga (pelvic utrasound) kwa ajili ya kutambua iwapo kiumbe kipo ama la, na kama kipo je ki hai ama kimekufa.
· Aidha ni muhimu pia kufanya uchunguzi wa magonjwa mbali ya zinaa ambayo husababisha mimba kutoka.
Matibabu ya utokaji wa mimba
Matibabu ya utokaji wa mimba hutegea sana aina ya utokaji wa mimba. Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia vitu vifuatavyo wakati wa kutoa matibabu kwa mtu aliyepoteza mimba
Wahudumu wa afya huzingatia kanuni zote (ABC) za kuokoa maisha ya mgonjwa kama vile
· kuhakikisha njia ya hewa ya mgonjwa ipo wazi na hewa inaingia na kutoka vizuri kwenye mapafu
·    kuhakikisha mgonjwa anapumua vizuri bila shida
·         kuhakikisha mishipa ya damu ya mgonjwa imewekwa mrija wa veni (intravenous line) na mgonjwa anapewa dripu ya maji ya normal saline.
·         kuhakikisha mgonjwa anaongezwa damu haraka iwapo vipimo vitaonesha kuwa alipoteza damu kwa wingi
Matibabu ya mimba inayotishia kutoka (threatened abortion)
Kwenye hali hii, mgonjwa hutakiwa             
·         kupumzika kitandani bila kufanya kazi yeyote (complete bed rest) angalau kwa wiki moja au zaidi mpaka hapo damu itakapoacha kabisa kutoka
·         kumpa ushauri na uhakika mama ili kumfanya atulie kiakili (assurance and proper councelling)
·         Mama pia hupewa dawa za kumtuliza na kumfanya apumzike (sedatives) kama vile phernobabitone
·         Aidha mama hupewa dawa kwa ajili ya kupunguza kusukuma kwa uterus (antispamodics) kama vile salbutamol
·         Kutofanya tendo la ndoa kwa wiki mbili au tatu
·         Aidha mama na mumewe hupewa ushauri juu ya tatizo hilo na jinsi ya kuendelea na matibabu
Matibabu ya mimba iliyotoka kamili (complete abortion)


Mara nyingi mgonjwa huwa haitaji matibabu zaidi ya uangalizi wa karibu kwa vile kiumbe pamoja na kondo lake la nyuma vyote huwa vimetoka kikamilifu. Mara chache sana, kulingana na jinsi daktari atakavyoona, mgonjwa anaweza kupewa antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi.
Matibabu ya utokaji wa mimba usiokuwa kamili (incomplete abortion)
Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba uhitaji mgonjwa kusafishwa kwa ajili ya kuondoa mabaki ya kiumbe (products of conception) yaliyobakia. Usafishaji huu huweza kufanywa kwa kutumia njia inayoitwa Manual Vacuum Aspiration (MVA).
Aidha mgonjwa hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa maambukizi ya vimelea vya bakteria.


Matibabu mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba ni pamoja na mgonjwa kuwekewa maji ya uchungu ili kiumbe kiweze kutoka. Wakati mwingine, daktari anaweza kuamua kusafisha mfuko wa uzazi (uterus) kwa kutumia njia inayoitwa dilatation and curettage. Sambamba na matibabu hayo, mgonjwa pia hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vimelea vya bakteria.


Matibabu ya tatizo la utokaji wa mimba unaojirudia (recurrent abortion)
Jambo la msingi katika matibabu ya tatizo la utokaji mimba unaojirudia (recurrent abortion) ni kugundua na kutambua chanzo kinachosababisha tatizo hilo na kisha kukishughulikia ili kuondoa kabisa kujirudia rudia kwa tatizo hili.