Kurasa

Friday, 31 October 2014

MAHABUSU WAMZODOA CHID BENZ




Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’ akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’ alijikuta akizodolewa na mahabusu wenzake mara baada ya kuingizwa katika Karandinga kupelekwa Segerea baada ya kukosa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 28, mwaka huu ambapo Chid Benz alikuwa akipelekwa Segerea huku mahabusu waliokuwemo ndani ya gari hilo wakitoa maneno ya kumkejeli pale alipokosa kiti na kulazimika kusimana.
Mmoja wa mahabusu alisikika akimzodoa Chid Benz kwa kumwambia: ‘Ustaa wako hukohuko, simama’ ambapo msanii huyo hakuleta ubishi, alisimama na safari ya kuelekea Segerea ikaanza. 

No comments:

Post a Comment