PENDA
ULAJI WA TIKITI MAJI
Licha ya 92% ya tikiti
maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo
linaloonekana kutofahamika kwa wengi.
Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni
miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio
tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.
Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye
faida kubwa katika afya ya mwanadamu.
Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A,
inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C,
inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli,
kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na
pia kuibadilisha protini kuwa nishati.
Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au
mboga za majani.
Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium,
unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na
mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la
damu.
Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha
mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia
kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi
yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa
tatizo hilo.
Kwa kawaida tunda hili huliwa peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti
maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.
No comments:
Post a Comment