Malaria ni maambukizo ya seli nyekundu za damu inayosababishwa na parasiti iitwayo Plasmodium . Plasmodium hawa husambazwa na mbu aina “Anopheles”.
Mbu huyu hutoa parasiti za malaria katika damu ya mtu alieambukizwa anaponyonya damu “chakula” na kasha kasha kupitisha parasiti anapomuuma mtu mwingine.
Parasiti hukua na kukomaa katika seli nyekundu za damu na mamilioni ya parasiti hukusanyika katika placenta ya mama mjamzito. Malaria inaweza kuwa kali zaidi kwa akina mama wakio na magonjwa mengine. Malaria ni hatari zaidi kwa wajawazito kuliko watu wengine.
DALILI ZA MALARIA KWA MAMA MJAMZITO
Mama mjamzito anakuwa na dalili kama wagonjwa wengine ambao sio wajawazito. Dalili hizo ni kama vile,
- 1. Baridi (kuhisi baridi isiyo ya kawaida) na kutetemeka kwa dakika kadhaa na hudumu hadi saa1) hii huwa dalili ya kanza ya maambuki.
- 2. Maumivu ya kichwa na udhaifui mara nyingi huandamana na baridi
- 3. Joto jingi mwilini (halijoto ya juu) joto jingi mwilini mara nyingi hufuatwa na baridi na joto linaweza kwenda juu sana hivyo mtu anakabiliwa na kuchanganyikiwa au kutokuwa sawa kiakili, kuona au kusikia mambo yasiyo halisi.
- 4. Kutokwa na jasho, joto lishukapo.
- 5. Katika baadhi ya hali zingine kuhara/ kutapika kunaweza pia kushuhudiwa.
- 6. Dalili nyingine ya kawaida ni maumivu ya misuli/ viungo
Hata hivyo magonjwa mengine yanaweza sababisha dalili kama hizi.
WIKI 12 ZA AWALI ZA UJAUZITO
Kwa kina mama wajawazito ambao hawana malaria kali dawa inayotumika kutibu malaria ARTESUNATE hutumika katika matibabu kwa muda wa siku saba.
MUHULA WA PILI WA MATIBABU
Dawa mseto jamii ya artemis zinaweza kutumika katika kipindi hivi hutibu malaria ambayo sio kali.
MADHARA YA MALARIA KWA MAMA MJAMZITO
Mama mjamzito aliye na malaria yuko katika hali ya kupata anemia, kuharubika kwa mimba (kutoka kwa mimba pekee yake kabla ya wiki 24 za ujauzito), kuzaa mapema, kupata mtoto mdogo zaidi, kuzaa mtoto aliyekufa (mtoto kuzaliwa akiwa amekufa baada ya wiki 24 za ujauzito) au kufa yeye mwenyewe (kifo cha mama mjamzito)
KUKINGA NA MALARIA
Kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii. Mama mjamzito afanyae kila awezalo kuepuka kuumwa na mbu.
Hata hivyo matumizi ya vyandarua pamoja na kuangamiza mazalia ya mbu hupunguza kuenea kwa ugonjwa wa kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii.
@ facebook: DOUGLAS MLATIE
@ tweeter: DOUGLAS MLATIE
No comments:
Post a Comment