Kurasa

Friday, 14 November 2014

FAHAMU KUWA SI KILA MWENYE KIFUA KIKUU ANA MAAMBUKIZO YA V.V.U

Mgonjwa mmoja, magonjwa mawili
          UKIMWI na kifua kikuu ni magonjwa mawili yanayosababisha vifo vingi, hivyo ni muhimu kuelewa uhusiano uliopo kati ya UKIMWI na Kifua kikuu.
              Virusi vya UKIMWI (V.V.U) Hupunguza kinga ya mwili na kuuacha mwili bila kinga ya kutosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa kifua kikuu.
Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaojitokeza baada ya upungufu wa kinga mwilini.
          Kuanzia miaka ya 1990s upungufu wa kinga mwilini unaosababishwa na maambukizo ya virusi vya UKIMWI (v.v.u) umetokea kuwa ni sababu kubwa ya ongezeko la ugonjwa wa kifua kikuu hasa watu wenye umri kati ya miaka 15-49. Umri huu unafanana na ule wa wengi walioathirika na maambukizi ya  V.V.U


MUINGILIANO HUU UNASABABISHA MGONJWA MMOJA KUWA NA MAGONJWA MAWILI UNATHIBITIKA KATIKA TAKWIMU AMBAPO;
  • ·      Asilimia 40-49 ya wagonjwa wa kifua kikuu hugunduliwa kuwa na VVU.
  • ·      Wastani wa asilimia 30 ya vifo vitokanavyo na UKIMWI nchini husababishwa na kifua kikuu.
  • ·      Mtu mwenye maambukizo ya VVU ana uwezekano wa mara 10 zaidi wa kuoata ugonjwa wa kifua kikuu ukilinganishwa na mtu ambaye hana VVU
  • ·      Magonjwa ya kifua kikuu na UKIMWI yakijitokeza pamoja hali ya mgonjwa huathirika zaidi, iwapo magonjwa yote haya hayatotibiwa pamoja, mgonjwa huchelewa kupona na huenda akapoyeza maisha yake.

KWA MGONJWA WA KIFUA KIKUU.
Kutokana na uhusiano kati ya kifua kikuu na UKIMWI , wagonjwa wote wa kifua kikuu wanapaswa kutambua iwapo wana maambukizi ya VVU.
Huduma hii ya kupima VVU hupatikana katika kituo chako au utapewa rufaa upate huduma hii katika kituo chako cha huduma/tiba ya walioathirika na VVU Iwapo haipatikani.


Ushauri nasaha na kupima VVU –DIAGONOSTIC COUNSELING AND TESTING (DCT)
Huu ni ushauri nasaha elekezi ambao mhudumu wa afya humnasihi mgonjwa kuhusu hali yake na faidi yakufanya uamzi wa kupima VVU. Baada ya kupima mgonjwa anapata fursa ya kufaidika na huduma zilizopo hata kama hana maambukizi ya VVU.

FAHAMU KUWA SI KILA MWENYE KIFUA KIKUU ANA MAAMBUKIZI YA V.V.U.
·      Ukiwa hukugundukulika kuwa na VVU; hii ni habari njema kwako na utashauriwa kuendelea na ushauri nasaha wa hiari VCT ili kuendelea kuishi bila ya maambukizi ya VVU, pia kumbuka unahitaji kuendelea na tiba simamizi ya kifua kikuu ambayo ni lazima kumaliza bila kuacha hata dozi kimoja
·      Ikiwa umegundulika una VVU; Ni habari njema kwako pia kwani kuifahamu hali yako kutakupa nafasi kubwa ya kutumia huduma shirikishi zilizopo na kuboresha afya yako.

UCHUNGUZI ZAIDI WA DAMU
Vipimo vikionyesha una maambukizo ya VVU utafanyiwa vipimo zaidi vya damu ili kutambua kiwango cha upungufu wa kinga yako ya mwili na kiasi cha maambukizo ya VVU ulichonacho mwilini.
Vipimo hivi vinamsaidia Daktari wako kuweza kuamua kama akuanzishie dawa za kupunguza makaili ya maambukizo ya VVU kulingania na kigezo cha kitaifa cha kuanza dawa hizi.

        DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA VVU.
Daktari ndie anayeamua kukuanzishia dawa za kupunguza makali  ya VVU kulingana na vipimo.
Utapewa dawa za mseto ambazo utazitumia kila siku na kwa kipindi cha maisha yako yote bila kukosa dozi.
Dawa hizi zitaboresha kinga ya mwili wako na kukufanya uweze kuendelea kuwa na afya na kufanya shughuli zako za kawaida pamoja na dawa za kifua kikuu, dawa hizi zitakusaidia kupona kifua kikuu kwa haraka zaidi.

        TIBA KAGAJI (PROPHYLAXIS)
Tiba hii hutolewa kwa mgonjwa wa UKIMWI au mwenye kifua kikuu/UKIMWI kujikinga na magonjwa nyemelezi.

KWA MGONJWA MWENYE MAAMBUKIZO YA VVU/UKIMWI
Maambukizi ya VVU hupunguza kinga ya mwili hivyo kumfanya alieathirika kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu wakati wowote.
Karibu asilimia 33 ya wenye VVU hugundulika kuwa na kifua kikuu, ni muhimu mwenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI kufanya uchunguzi wa kifua kikuu mara kwa mara.

        IWAPO UTAONYESHA UNA KIFUA KIKUU
Utaanzishiwa dawa za kifua kuu chini ya usimamizi, dawa hizi ni za mseto na utameza kila siku bila kukosa kwa muda wa miezi sita.
        Utachagua ni wapi utamezea dawa chini ya usimamizi, katika kituo cha huduma ya afya au katika jamii yako
        Dawa za kifua kikuu hutolewa bure bila malipo yoyote
        Baada ya kukamilisha matumizi ya dawa za kifua kikuu na kupona utaendelea na huduma za dawa za kupunguza makali ya VVU za ARVs ( ikiwa ulikuwa na Kifua kikuu pamoja na UKIWMI)
  • BORESHA AFYA YAKO KAMA UNA KIFUA KIKUU AU KIFUA KIKUU/UKIMWI
  •       AMUA; mapema kufanya uchunguzi zaidi wa afya yako ili kufahamu kama una ugonjwa mmoja au magonjwa yote
  •    TUMIA DAWA ZA MSETO; kila siku bila kukosa kama ulivyoelekezwa na wataalamu wa afya, wahi kutoa taarifa katika kituo chako cha huduma iwapo utakuwa na tatizo lolote wakati wa huduma.
  •       LISHE; kula vyakula mchanganyiko kwani mwili wako unahitaji kuwa na nguvu, kujijenga na hasa kuijenga kinga ya mwili ili kusaidia dawa kupambana na vimelea vya magonjwa.
  •      JENGA TABIA; ya kutafuta habari za elimu ya afya kwa kusoma Blog kama hii ya masuala ya afya, vyombo vya habari, majarida ya afya na kuhudhuria vipindi vya elimu ya afya katika kituo chako cha huduma.
  •       JENGA MAHUSIANO ya kuwa karibu na wasimamizi wa kumeza dawa na wataalamu wa afya ili kupata elimu na ushauri kuhusu maendelea ya Afya yako.

“pambana na kifua kikuu pambana na UKIMWI”
Pambana sasa

WANAMICHEZO NYAMA NI MUHIMU ILA TUSIZIDISHE KIWANGO CHA ULAJI

 Tunaposema nyama tunamaanisha misuli iliyopo kwenye mwili wa mnyama ambapo hutumika kama chakula kwa binadamu na hata kwa wanyama wanaokula nyama kama vile Simba, Chui, Mbwa na wanyama wengine wengi tu.
Kwa binadamu nyama tunazokula ni kwa baadhi ya wanyama tu, ingawaje kuna wengine wanakula kila kitu mpaka nyama ya nyoka na pengine hata binadamu wenzao. Pamoja na misuli pia viungo kama maini, moyo, figo, ubongo pia huweza kutumika kama kitoweo kama nyama.

Nyama hapa ulimwenguni huweza kupatikana toka kwenye wanyama kama Ng’ombe, Kondoo, Mbuzi, sungura nk. Hali kadhalika kuna wanyama wa porini kama Nyumbu, Nyati, Swala, Digidigi nk. Mila na desturi pia zinachangia kwenye suala hili la kufanya nyama kuwa kitoweo.

Ni kawaida kwa wanamichezo mbalimbali hapa ulimwenguni mara baada ya kutoka mazoezini au kwenye mashindano kupata chakula ambacho kimeandaliwa vizuri ikiwa ni pamoja na kuwa na kiasi fulani cha nyama kama supu, mboga iliopikwa, kukaangwa, kuokwa na hata nyama choma kama mishikaki au hata mazao ya nyama kama vile soseji,kababu nk.

Nyama na mazao yake ni chanzo muhimu sana cha protini yenye kiwango cha hali ya juu hapa ulimwenguni. Uwepo wa amino acids katika nyama unamchango mkubwa katika kuhakikisha walaji ikiwa ni pamoja na wanamichezo wanapata protini iliyopo kwenye nyama wakati wanapokula vyakula vingine vya jamii ya nafaka, ambavyo hutumika kama vyakula vyao vya kila siku kwenye maeneo wanayoishi.

Nyama inapoliwa huweza kuongeza madini ya chuma ambayo huwa yanafyonzwa kirahisi mno na pia kusaidia ufyonzwaji wa madini hayo ya chuma yaliyopo kwenye vyakula vingine, huku pia ikisaidia ufyonzwaji wa madini ya zinki. Nyama na mazao yake pia ni chanzo muhimu sana cha lile kundi la vitamin B.

Wanamichezo wanapokula nyama na mazao yake huweza kutoa mchango mkubwa sana katika kuondosha matatizo mbalimbali ya lishe kwenye miili yao, ingawa ulaji wa nyama kwa kiasi kikubwa umekuwa ukihusishwa na matatizo ya kiafya kama vile ugonjwa wa gout, kupotea kwa madini ya calcium toka kwenye mifupa, kutokea kwa vijiwe kwenye figo(kidney stones), na kibaya zaidi ni tatizo la ongezeko la mafuta mwilini na lehemu(cholesterol).
 
Unapokula kiasi kikubwa cha nyama ambayo ndani yake kuna saturated fatty acids hupelekea kupandisha kiwango cha lehemu(cholesterol) kwenye mkondo wa damu na hivyo kujilimbikiza katika mishipa ya damu na kuifanya kuta zake zisinyae kiasi cha kupitisha damu kwa shida zaidi au hata kutopitisha kabisa damu kuelekea kwenye viungo vingine na kupelekea kujitokeza kwa magonjwa ya moyo, mashambulio ya moyo, kiharusi nk.

Maeneo mengi hapa ulimwenguni ambako nyama ndio chakula kikuu, inasemekana karibu robo ya saturated fatty acids huwa inatokea kwenye nyama inayoliwa katika milo mbalimbali iliyo rasmi na isiyo rasmi, na hii imeweza kutumiwa na baadhi ya taasisi kupiga vita ulaji wa nyama hasa nyama nyekundu.
Ingawaje masuala haya ya ulaji nyama kwa kiwango kikubwa yameonekana zaidi katika nchi za magharibi, ambako nyama huweza kuliwa kwa kiasi kikubwa kila siku iendayo kwa Mungu, sambamba na vyakula ambavyo vina kiwango kikubwa cha saturated fatty acids, ikiwa ni pamoja na vile vinavyotengenezwa viwandani, kwenye migahawa na mahoteli makubwa. Huku kwetu kwenye nchi ambazo hazijaendelea, hali ni tofauti kidogo. 

Hali kadhalika mbali na ulaji wa nyama kwa kiwango kikubwa pia kuna vitu vingi ambavyo vinahusishwa na magonjwa ya moyo na hata kiharusi, ikiwa ni pamoja na historia ya familia kwa ujumla, uvutaji wa sigara na bangi, madawa ya kulevya, ugonjwa wa kisukari, tabia binafsi ya kupuuzia kufanya mazoezi, shinikizo la damu na hali ya magonjwa mengine.

Kiwango kikubwa cha lehemu(cholesterol) kinatokana na ulaji wa kiwango kikubwa cha nyama hasa yenye mafuta mengi, maziwa na viini vya yai, japokuwa ukivikosa kabisa vyakula hivi unapata matatizo ya lishe duni. Hivyo vyakula hivi vya jamii ya nyama, maziwa na viini vya yai ni vya muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku, kinachotakiwa tusizidishe kiwango cha ulaji wa vyakula hivi. Hasa kwa wale watu ambao wanahisiwa wanaweza kuathirika na ulaji wa vyakula hivyo ambao tayari wana vitambi na unene uliopitiliza.

Kwa kifupi miongozo mingi ya lishe hapa ulimwenguni inapendekeza, kupunguzwa kwa vyakula vinavyochangia kwa kiwango kikubwa cha lehemu(cholesterol) yaani ulaji wake angalau usizidi miligramu 300 kwa siku, huku kiwango kinachoshauriwa kwa siku cha protini inayohitajika mwilini ni gramu 45 hadi 60.

Inafikiriwa kuwa kwa sasa vyakula vyenye mafuta hasa yenye kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) havina budi kudhibitiwa kwa jamii na wanamichezo ili kujiepusha na magonjwa ya moyo na kiharusi. Maeneo mengine hapa ulimwenguni, miongozo ya lishe inapendekeza kuwa badala ya kula kwa wingi nyama ya ng’ombe ambayo ni nyama nyekundu basi nyama nyeupe kama vile ya kuku,bata na zingine zitumike.

Zipo pia faida za kutokula nyama kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na kurefusha maisha, kuepuka magonjwa ya moyo na kiharusi, kuepuka magonjwa ya kisukari, kansa, kuepuka mashinikizo ya damu,mwili kuwa na uzito sahihi na mwili kuwa na kiwango stahiki cha lehemu(cholesterol).
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Afya ya Taifa nchini Marekani, umebaini kuwa watu wanaopenda kula kwa wingi nyama nyekundu, hufa mapema kuliko wale wanaokula kiasi kidogo cha nyama hiyo.

Wapenda nyama ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupatwa na saratani na ugonjwa wa moyo ni wale wanaokula kuanzia kiasi cha gramu 112 za nyama (karibu robo kilo) kila siku, lakini wanaokula kiwango kidogo (nusu ya robo kilo) hawako hatarini na badala yake watapata virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye nyama.

Ulaji wa nyama nyekundu wenye faida kwa mwili wa binadamu ni ule unaozingatia kiasi na aina ya nyama. Nyama inayopendekezwa ni steki isiyo na chembe ya mafuta (lean meat) na itakayoliwa kwa kiasi kidogo.

Nyama inahitajika kiafya kwa sababu ina madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa wasichana na wanawake wanaotarajia kuzaa. Pia nyama ina Vitamini B12 ambayo husaidia utengenezaji wa DNA na hujenga mishipa na seli za damu. Halikadhalika kuna madini ya zinki ambayo husaidia kuimarisha ufanyaji kazi wa kinga ya mwili. Bila kusahau nyama ina protini ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa mifupa na misuli.

Kwa ujumla, nyama nyekundu ni muhimu kwa afya ya binadamu, lakini itakuwa muhimu kama itatumiwa kwa kiwango na kiasi kinachotakiwa. Siku zote wanamichezo  waepuke kula nyama yenye mafuta na badala yake wapendelee kula steki isiyokuwa na mafuta ili upate virutubisho vyake muhimu kwa afya yako.

Kula nyama kinyume na mwongozo huu, ni sawa na kuamua kujiweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo na matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo ugonjwa wa miguu au kansa ya tumbo. Tumekuwa tukishuhudia vifo vya ghafla kwa wanamichezo pindi wanapokuwa uwanjani kutokana na matatizo mbalimbali ya moyo ikiwa ni pamoja na mashambulio ya moyo.

Tumeshuhudia pia Fabrice Muamba mchezaji wa timu ya Bolton Wanderers ambae alilazwa katika kituo cha mshituko wa moyo cha London Chest Hospital akiwa katika hali mahututi", kutokana na kuanguka ghafla akiwa mchezoni, hali iliyompelekea astaafu kucheza soka ili kunusuru maisha yake.

Wanamichezo hawanabudi wajiepushe na ulaji wa nyama na vyakula vingine vyote vinavyoweza kupelekea wapatwe na matatizo ya kiafya kwa kiwango kikubwa kwa kuzingatia masharti ya ulaji sahihi. Kama nilivyokwisha sema kuwa nyama ni tamu na muhimu ila tule kwa kiasi ili kuzinusuru afya zetu.

KULALA CHALI KWA MJAZITO NI HATARI KWA MTOTO

Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali  wapo kwenye hatari  ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi.
Katika utafiti  uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito  walikuwa  kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na  kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.


Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu.Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya  watoto wafu wanaozaliwa  katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.

Mkuu wa utafiti huu,Louise O'Brien  kutoka chuo kikuu cha Michigan, nchini Marekani amesema kama kutokulala chali wakati wa ujauzito hupunguza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu basi ni vizuri kuhamasisha kina mama wajawazito kutolala chali kwani hii ni njia rahisi na isiyokuwa na gharama yoyote ile.
Tabia hii ya kulala chali wakati wa ujauzito inaweza kuepukika kwa kuwashauri  kina mama wajawazito madhara yanayopatikana kwa kulala chali.
Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha ya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watoto wanaozaliwa wafu inaweza kuepukika kwa kubadilisha staili ya kulala tu kwa wanawake wajawazito.

Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.


          Utafiti huu uliofanyika nchini Ghana unaunga mkono utafiti uliofanyika hivi karibuni nchini Australia unaojulikana kama Sydney Stillbirth Study ambao ulisema ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito wako kwenye hatari ya mara sita zaidi ya kuzaa watoto wafu.Utafiti huu wa Australia ulifanyika kwa miaka mitano na ulihusisha wanawake wajawazito 295 kutoka katika hospitali nane nchini Australia. 

Naye mtafiti mkuu katika utafiti huu Dr. Adrienne Gordon, kutoka Sydney's Royal Prince Alfred Hospital amesema “Tafiti za awali zilionyesha ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito, hupunguza mzunguko wa damu unaotakiwa kwenda kwa mtoto.Lakini  pia ni vizuri kwa wanawake ambao ni wajawazito  kutotaharuki kama wakati mwingine watalala chali.’’Kutokana na idadi ndogo ya wanawake wajawazito waliohusishwa kwenye utafiti huu sisi wana Tanzmed tunachelea kusema ya kwamba ni vigumu kusema utafiti huu umetoa mapendekezo sahihi ya  namna ya kulala kwa wanawake wajawazito.

Pia kutokana na kutoangalia muda ambao wanawake hao walilala wakiwa chali (mfano kama walilala masaa 4,6 au 8 kwa siku na kwa siku ngapi) na tofauti ya hatari kati ya wanawake wajawazito waliolala muda mfupi na mrefu, hivyo tunawaambia wanawake wajawazito kutohofu kama watalala chali lakini ni bora kuchukua tahadhari mapema.Tafiti hii inatoa changamoto kwa watafiti wetu wa afya kuangalia jinsi ya kufanya tafiti kama hizi katika mazingira ya kwetu.

UGONJWA WA MALARIA KWA MAMA MJAMZITO

Malaria ni maambukizo ya seli nyekundu za damu inayosababishwa na parasiti iitwayo Plasmodium . Plasmodium hawa husambazwa na mbu aina “Anopheles”.

Mbu huyu hutoa parasiti za malaria katika damu ya mtu alieambukizwa anaponyonya damu “chakula” na kasha kasha kupitisha parasiti anapomuuma mtu mwingine.
Parasiti hukua na kukomaa katika seli nyekundu za damu na mamilioni ya parasiti hukusanyika katika placenta ya mama mjamzito. Malaria inaweza kuwa kali zaidi kwa akina mama wakio na magonjwa mengine. Malaria ni hatari zaidi kwa wajawazito kuliko watu wengine.

DALILI ZA MALARIA KWA MAMA MJAMZITO
Mama mjamzito anakuwa na dalili kama wagonjwa wengine ambao sio wajawazito. Dalili hizo ni kama vile,
  • 1.   Baridi (kuhisi baridi isiyo ya kawaida) na kutetemeka  kwa dakika kadhaa na hudumu hadi saa1) hii huwa dalili ya kanza ya maambuki.
  • 2.   Maumivu ya kichwa na udhaifui mara nyingi huandamana na baridi
  • 3.   Joto jingi mwilini (halijoto ya juu) joto jingi mwilini mara nyingi hufuatwa na baridi na joto linaweza kwenda juu sana hivyo mtu anakabiliwa na kuchanganyikiwa au kutokuwa sawa kiakili, kuona au kusikia mambo yasiyo halisi.
  • 4.   Kutokwa na jasho, joto lishukapo.
  • 5.   Katika baadhi ya hali zingine kuhara/ kutapika kunaweza pia kushuhudiwa.
  • 6.   Dalili nyingine ya kawaida ni maumivu ya misuli/ viungo

Hata hivyo magonjwa mengine yanaweza sababisha dalili kama hizi.


WIKI 12 ZA AWALI ZA UJAUZITO
Kwa kina mama wajawazito ambao hawana malaria kali dawa inayotumika kutibu malaria ARTESUNATE hutumika katika matibabu kwa muda wa siku saba.
MUHULA WA PILI WA MATIBABU
Dawa mseto  jamii ya artemis zinaweza kutumika katika kipindi hivi hutibu malaria ambayo sio kali.


MADHARA YA MALARIA KWA MAMA MJAMZITO
Mama mjamzito aliye na malaria yuko katika hali ya kupata anemia, kuharubika kwa mimba (kutoka kwa mimba pekee yake kabla ya wiki 24 za ujauzito), kuzaa mapema, kupata mtoto mdogo zaidi, kuzaa mtoto aliyekufa (mtoto kuzaliwa akiwa amekufa baada ya wiki 24 za ujauzito) au kufa yeye mwenyewe (kifo cha mama mjamzito)



KUKINGA NA MALARIA
Kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii. Mama  mjamzito afanyae kila awezalo kuepuka kuumwa na mbu.
Hata hivyo matumizi ya vyandarua pamoja na kuangamiza mazalia ya mbu hupunguza kuenea kwa ugonjwa wa kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii.

@ facebook:  DOUGLAS MLATIE
@ tweeter: DOUGLAS MLATIE

FAIDA ZA KIAFYA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO

NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO.
Kunywa kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi inaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati.

Wengi wetu huianza asubuhi vyema kwa kikombe safi cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa lengo la kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani. Pale tunakunywa maji, basi wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini kutokana na watalaam wa afya wanavyosema,  tunafanya makosa kufanya hivyo. Mara nyingi unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani majira ya asubuhi, inasaidia kuiponya miili yetu na kuitibu,
kwa kusaidia kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwili ambazo zinaweza kuzuia kinga zetu kuwa katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi.
“matabibu wanasema na kushauri kunywa maji moto ama uvuguvugu nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanyanyo wa maji ya limao, au chai ambayo haina madhara kwa mwili” anasema stella metsovas. Mtaalam katika masuala ya lishe na sayansi ya vyakula alipokuwa akiliambia jarida la Medical Dail.

Utumiaji wa maji moto ama vuguvugu huongeza ukazwaji wa utumbo, ambapo husaidia uondoaji wa vitu visivyotakiwa. Tofauti na maji moto, utumiaji wa maji ya baridi yenyewe huzuia vitu muhimu ikiwemo madini ambayo huwa si rafiki kwa mazingira hayo katika mfumo wa umeng’enywaji unapokula chakula.

Kwa wanywaki wa maji ya baridi, metsovas anashauri kutangulia kunywa maji hayo ya baridi dakika 20 kabla ya kula hata kama maji hayo yanatoka katika vyanzo vya asili vya maji. Wakati unywaji wa maji ya moto ama vuguvugu yanaweza yasiwe mazuri kwa radha yanapokuwa mdomoni,

Hizi hapa zifuatazo ni sababu kwanini unywa maji haya ya uvuguvugu,

1.  Hurahisisha umeng’enywaji wa chakula,
Maji ya moto ama vuguvugu katika kikombe uamkapo asubuhi inaweza kukusaidia mwili wako kuweza kutoa nje sumu katika mwili wako. Maji na vimiminika vingine husaidia kuvunja vunja chakula katika tumbo na kuweka mfumo wa chakula kuwa katika hali nzuri ndani ya mwili. Maji moto au vuguvugu husaidia kuweza kuvunja vunja chakula hicho kwa uharaka zaidi, na hivyo umeng’enywaji wa chakula kuwa mwepesi na kwa haraka.
Unywaji wa maji ya baridi wakati wa ama baada cha mlo wako inaweza kusababisha kusaidia kugandishwa kwa mafuta ambayo unayapata kupitia chakula na hivyo kusababisha mrundikano wa mafuta katika utumbo.
Uongezwaji wa barafu ili kutengeneza maji ya baridi hufanya kubadili mfumo halisi wa madini na virutubisho katika mwili, anasema Metsovas, ambavyo madini hayo ni muhimu ili kuweza kuuweka mfumo wa chakula katika hali ya afya, ambadani unaweza kufanya njia mbadala kwa kunywa chupa ya maji ya baridi sambamba na chupa ama glasi ya maji ya uvuguvu au moto ili kusaidia umeng’enywaji wa chakula, hususani baada ya kula mlo wako.
3. husaidia kulainisha choo
Kwa pointi moja au nyingine, wengi wetu tunakabiliwa na vidonda hususani matatizo ya tumbo ambapo huwa na choo kidogo au kukosa kabisa haja kubwa.
Vile vile ugumu wa haja uendapo choo wakati wa kukitoa, husababisha kuchanika kwa eneo la haja kubwa, haya yote yana letwa na ukosefu wa maji katika mwili. Unywaji wa maji moto au vuguvugu nyakati za asubuhi wakati tumbo likiwa halina kitu inaweza kusaidia utumbo mpana kuweza kusukuma uchafu/ kinyesi vyema na hivyo kusaidia kuwe na choo laini {kinyesi chepesi} wakati wa uvunjwaji wa chakula na hata usafirishwaji wake huwa mzuri kupita katika utumbo. Hivyo uchangamshwaji wa utumbo na maji moto husaidia kuurudisha mwili katika ufanyaji wake mzuri na wakawaida wa kazi vyema.

3. huodoa maumivu

Maji ya moto au vuguvugu, tukizingatia ni maji asilia ambayo wengi wetu katika majumba hutumia, husaidia kuondoa maumivu ya tumbo la hedhi kwa wakina mama na maumivu ya kichwa.

Umoto toka kwenye maji moto huweza kuwa na athari chanya katika misuli ya tumbo, ambayo huweza kusaidia kuondoa papo kwa papo makazo na misuli kujinyoosha. Kwa mujibu wa Healthlinewanasema maji moto au vuguvugu ni mazuri kwa maumivu, na kimiminika cha moto huongeza mzunguko wa damu kwenye ngozi na hivyo kusaidia kushusha maumivu ya misuli.

4. Husaidia kupunguza uzito

Kama uko katika mlo wako, unywaji wa maji nyakati za asubuhi basi inaweza kukusaidia katika kupunguza uzito. Maji moto ama uvuguvugu husaidia kuongeza joto la mwili, ambapo huongeza metabolic/ kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili. Kadiri kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili kinapoongezeka huruhusu mwili kuweza kuchoma kalori nyingi katika mwili. Hivyo husaidia figo na gastrointestinal kufanya kazi vyema katika mwili.

 “madaktari wana shauri kuwa unywaji wa maji moto nyakati za asubuhi, kila siku, pamoja na limao ndani yake, au chai huondoa vitu hatari katika mwili”.anasema Metsovas. Unywaji wa glasi kadhaa za maji ya moto au vuguvugu na limao ndani yake husaidia kuvunja vuja tisu za mafuta, katika mwili na hivyo husaidia mmeng’enyo wa chakula.
5. Huboresha mzunguko wa damu

Mrundikano wa mafuta katika mwili huondolewa wakati wa unywaji wa maji ya moto. Hii husaidia kuondoa sumu ambazo huwa zimezunguka katika miili yetu kwa kufanikisha mzunguko wa damu.
 Hakikisha misuli inapumzika na hivyo wakati kunapokuwa na mzunguko mbovu wa damu katika mwili wako.

6. Hupunguza hatari ya kuzeeka mapema

Hii inaweza kuzuilika kwa kunywa maji moto ama vuguvugu, upatikanaji wa sumu katika mwili hupelekea kuzeeka mapema na kwa haraka, lakini maji moto ama vuguvugu inaweza kusaidia kusafisha mwili kwa kutoa hizo sumu, hata hivyo pia kuirekebisha ngozi kwa kuoneza SelI mpya maeneo ya ngozi. Metsovas aliliambia jarida la Medical Daily  “wanawake siku zote hunufaika kwa sababu wanakuwa na homoni nyingi zaidi ambazo huhusika kwayo,”

          Kuweza kuwa ama kuongeza uimara wa afya yako kupitia unywaji wa maji moto ama vuguvugu, kunywa kila siku asubuhi maji pekee au yaliyochanganywa na limao kwa kuongeza radha. Metsovas anakubaliana na wanywaji wa maji vuguvugu au moto kwa, kadiri wanavyokunywa  maji moto wanaweza kuwa wana angamiza tisu za mdomo na hata maeneo ya kolomeo.  Baada ya kuuguzwa na maji hayo ya moto,
          Basi huna budi kuyaacha yapoe kidogo kabla ya kuanza kuyatumia kwa kuyanywa.

          Vile vile anashauri “ kila mara mwone daktari kwa maelezo kabla ya kuanza kunywa  maji hayo ya moto, kama utakuwa katika matumizi mengine ya dawa ambayo inaweza kuleta madhara katika ufanisi wa dawa hiyo” anasema metsovas.

@ facebook:  douglas mlatie
@tweeter : douglas mlatie