Kurasa

Wednesday, 3 December 2014

SETHI TEGETE ESCROW NAMWACHIA MUNGU

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi
Wakati masikio ya Watanzania yakiwa yameelekezwa Ikulu kusikia maamuzi ya Rais Jakaya Kikwete juu ya maazimio manane yaliyotolewa na Bunge kuhusu sakata la uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi, ameibuka na kudai kuwa anamuachia Mungu yote yaliyotokea.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwa simu katika mahojiano maalum na NIPASHE kuhusu mambo yaliyojitokeza katika mkutano wa16 na 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakati wabunge walipokuwa wakijadili kashafa ya uchotaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

No comments:

Post a Comment