Kurasa

Wednesday, 3 December 2014

SETHI TEGETE ESCROW NAMWACHIA MUNGU

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi
Wakati masikio ya Watanzania yakiwa yameelekezwa Ikulu kusikia maamuzi ya Rais Jakaya Kikwete juu ya maazimio manane yaliyotolewa na Bunge kuhusu sakata la uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi, ameibuka na kudai kuwa anamuachia Mungu yote yaliyotokea.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwa simu katika mahojiano maalum na NIPASHE kuhusu mambo yaliyojitokeza katika mkutano wa16 na 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakati wabunge walipokuwa wakijadili kashafa ya uchotaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

MTANDAO WA ZARI ALIOPITIA KABLA YA DIAMOND

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady.Kwa mujibu wa jarida la linalodili na habari za showbiz (biashara ya shoo) la E-Vibe la nchini Uganda la hivi karibuni, Zari ambaye wikiendi iliyopita alimng’arisha Diamond katika zulia jekundu kwenye Tuzo za Channel O (Choamva) zilizofanyika Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz’, anadaiwa kuwa ‘klozi’ na idadi hiyo ndefu ya wanaume.Stori: Sifael Paul
Ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha kila kukicha, mrembo tajiri mwenye maskani yake nchi jirani ya Uganda na Afrika Kusini, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, anadaiwa kuwa na mtungo mrefu wa wanaume ambapo kama ni kweli anatoka na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ basi jamaa huyo atakuwa anashika nambari 13.

MAASKOFU WA ESCROW! KILAINI, NZIGIRWA, TWIMANNYE NITAUNGAMA NIKIWATAZAMA USONI

Baba Askofu Methodius Kilaini akitoa huduma kanisani. UKIHOJI dhambi za viongozi wa dini harakaharaka utaambiwa fuata mafundisho yao usifuate matendo. Hili ni kinyume na Mtume Paul aliyefundisha waumini wake kuwa wamfuate yeye kama alivyomfuata Yesu. 

Kwa kuwa dini ni muhimu kwenye kaya yangu sibishi sana katika hilo, lakini kuhusishwa kwenye fedha chafu kwa viongozi wa dini Askofu Methodius Kilaini, Euesebius Nzigirwa na Alphonce Twimannye kumenibadilisha mtazamo. 
Sikuwahi kuuliza utakatifu wa viongozi hao wa dini kwa sababu za kutofuata matendo yao; lakini sakata la ufisadi wa Escrow wa zaidi ya shilingi bilioni 300 limenifanya nijiulize kimoyomoyo watawa hawa walipewa fedha hizo kwa ajili ya kazi gani?
Swali hili lipo na litaendelea kuwepo kwa sababu Mkuu wa Kaya sijapata majibu ya msingi. Kwa hali hiyo, hata nitakapokwenda kuungama dhambi zangu mbele ya watumishi hao wa Mungu nitakuwa nawatazama usoni. 

MTUNISI WA BONGO MUVI AKIONA CHA MOTO MAHAKAMANI!

Msanii nyota wa filamu Bongo, Nice Mohammed maarufu kama Mtunisi. Mtunisi alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, ambapo baada ya kusomewa shtaka lake la kushambulia mwili, mtuhumiwa alikana na hivyo hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena.Hata hivyo,

SHILOLE ALIVYONOGESHA UBELGIJI‏


Shishi Baby akifanya mambo yake huku mashabiki wakiwa na midadi.

ZITTO AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE KIGOMA


Tuesday, 2 December 2014

Manchester United vs Stoke City, Premier League



Manchester United 1 - 1  Stoke City, Premier League: HALF TIME

YAYA TOURE AONGOZA WATANO WALIOINGIA FAINALI KUSAKA TUZO MCHEZAJI BORA AFRIKA 2014

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya mwisho ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka huu kutoka kwenye orodha ya awali iliyokuwa na wachezaji 25.
yaya
Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure anaongoza orodha hiyo ya nyota watano akitarajiwa kuitwaa kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuinyakua pia msimu uliopita.
Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Wanigeria Vincent Enyeama na Ahmed Musa; Mghana Asamoah Gyan na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon.
Toure alitwaa tuzo hiyo miaka mitatu iliyopita na kama akifanikiwa kuitwaa tena msimu huu, atakuwa amefikia rekodi ya Mcameroon Samuel Eto, ambaye ameitwaa mara nne.
Mshindi atatangazwa jijini Lagos, Nigeria Alhamis Januari 8, 2015.


MANENO YA ZARI KUHUSU DIAMOND PLATZNUM


VIDEO DIAMOND NA ZARI WALIVYOACHA GUMZO AFRIKA KUSINI 2014


BOFYA KUIOA VIDEO KAMILI>>

DIAMOND PLATNUMZ ATUA DAR, APATA MAPOKEZI YA KUTISHA


Diamond baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.
MWANAMUZIKI Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametua nchini muda huu akitokea Afrika Kusini alipokwenda kushiriki zoezi la utoaji tuzo za Channel O ambapo alijinyakulia tuzo tatu kwa mpigo. Tuzo alizonyakua staa huyo ni pamoja na Most Gifted New Comer, Most Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number One. 

PICHA ZAIDI MAPOKEZI YA DIAMOND LEO DAR KUTOKA AFRIKA KUSINI