Kurasa

Tuesday, 2 December 2014

YAYA TOURE AONGOZA WATANO WALIOINGIA FAINALI KUSAKA TUZO MCHEZAJI BORA AFRIKA 2014

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya mwisho ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka huu kutoka kwenye orodha ya awali iliyokuwa na wachezaji 25.
yaya
Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure anaongoza orodha hiyo ya nyota watano akitarajiwa kuitwaa kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuinyakua pia msimu uliopita.
Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Wanigeria Vincent Enyeama na Ahmed Musa; Mghana Asamoah Gyan na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon.
Toure alitwaa tuzo hiyo miaka mitatu iliyopita na kama akifanikiwa kuitwaa tena msimu huu, atakuwa amefikia rekodi ya Mcameroon Samuel Eto, ambaye ameitwaa mara nne.
Mshindi atatangazwa jijini Lagos, Nigeria Alhamis Januari 8, 2015.


No comments:

Post a Comment