Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu
ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika
mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000
iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye
vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi
mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika
mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Historia inaonesha kuwa, vitunguu
swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa
Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na
wakulima barani Afrika walivitumia sana.
Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi
wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua
vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza
kutumika kama dawa ya kusafishia
vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia.
Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii
ya
vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya
kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo
kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.
Faida za vitunguu swaumu
Katika tafiti mbalimbali vitunguu
swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na
virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo
kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha
shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na
Kutibu saratani ikiwemo saratani ya
tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani
katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa
wingi.
Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti
kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa
kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi
mpaka watakaposhauriwa na daktari.
Huzuia kusanyiko la chembe sahani
zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo
kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
Ina kiasi kikubwa cha vitamini C
ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi
kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.
Ushahidi wa Kitafiti
Katika utafiti uliofanyika nchini
Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika
kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini
(low
density lipoproteins) katika mishipa
ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia
kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua
iliyosababishwa na virusi. Mwaka
2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo
la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu
yaliyozoeleka ya dawa na njia
nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu
shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati
wengine walipewa dawa isiyohusika na
matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa
vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo
mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza
kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure,
tofauti na wale waliopewa placebo.
Nini siri ya kitunguu swaumu?
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu
swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na
viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake
wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
Vina uwezo wa kusababisha kutanuka
kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani
yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
Husaidia uthibiti wa kiwango cha
sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza
madhara ya kisukari.
Iwapo vitapondwa pondwa vizuri,
vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria,
na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu
hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.
Nini Madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu
pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana
na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza
kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza
kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
Huweza kusababisha hatari ya kuvuja
damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda
kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito,
baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
Huingiliana katika utendaji kazi wake
na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo
la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya
quinolone kama vile ciproflaxacillin.
Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara
kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
FAIDA YA KITUNGUU SAUMU KINATIBU
MARADHI MENGI BINADAMU ANAJISAHAU KUTUMIA KITUNGUU SAUMU.
Kitunguu swaumu hakikosekani katika
kila jiko duniani.Ni mmea maarufu sana kwa tiba.Kitunguu swaumu ni jamii ya
yungiyungi.Kitunguu swaumu kilicho bora zaidi duniani ni kinachotoka misri
kwasababu ya tabia ya ardhi yake na mto nail.Kitunguu swaumu kina harufu ya
kipekee isiyowapendeza watu wengi ingawa kimebeba siri nyingi za tiba.Kwa ajili
hiyo maana yake kilatini ni HARUFU ICHOMAYO.
Ili kuepukana na harufu ya kitunguu
swaumu baada ya kukila,kula tofaa au tafuna majani mabichi ya naanaa,au kunywa
maji yaliyotokosewa karafuu.Kitunguu swaumu kitapoteza nguvu ya tiba iwapo
kitapikwa na kila kinapowekwa muda mrefu ndipo nguvu zake huongezeka (baada ya
majani yake kukauka kabisa).
Kitunguu swaumu kimekusanya protin
49%,sulphur 25%,kiasi fulani cha chumvi,homoni zitoazo nguvu za kiume,viuaji
sumu,vikojozavyo,vitoavyo safura,vinavyoteremsha hedhi,vimeng'enyo vyenye
kuyeyusha mafuta na viini vyenye kuua minyoo.Kila utafiti unapoendelea ndipo
faida na maajabu ya kitunguu swaumu yanapoongezeka.
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA
KITUNGUU SWAUMU;
1.Kiua sumu
2.Kisafisha tumbo
3.Kiyeyusha mafuta(cholestro)
4.Huzuia mvilio wa damu
5.Kusafisha njia ya mkojo
6.Kutibu amoeba
7.Kuzuia kuhara damu(Dysentery)
8.Tumbo kushindwa
kumeng'enya(Indigestion)
9.Gesi
10.Msokoto wa tumbo
11.Typhoid
12.Kidonda kilichooza
13.Dondakoo
14.Mabaka
15.Baridi yabisi(Rheumatisim)
16.Mishipa
17.Uziwi
18.Virusi vya homa ya
mafua(Influenza)
19.Mafua
20.Saratani(Cancer)
21.Kifaduro
22.Kifua kikuu cha mapafu
23.Kipindupindu
24.Kutoa minyoo
25.Upele
26.Kuvunjavunja mawe katika figo
27.Mba kichwani
28.Kuupa nguvu ubongo
29.Kuupa nguvu fizi
30.Kuzuia meno kung'ooka
31.Nguvu za kiume
32.Maumivu ya kichwa
33.Kizunguzungu/kisunzi
34.Kutuliza maumivu ya meno
35.Kujenga misuli na kutia nguvu
36.Mkakamo wa ateri(Arteriosclerosis)
37.Shinikizo la damu
38.Kinga ya tauni na ukimwi
39.Magonjwa ya macho
KITUNGUU SAUMU
kimekuwa kikitumika kutibu na kuboresha
afya ya mwili na hivyo kumfanya mtumiaji awe mrembo na mwenye afya bora.
Matumizi ya kitunguu saumu kibichi
yamekuwa yakisaidia vitu vingi sana mwilini.
Baadhi ya hayo ni pamoja na kupambana
na virusi, bakteria, fangasi na pia sumu mbalimbali hasa zile zinazosababishwa
na baadhi ya vyakula mwilini.
Kutokana na hilo, matumizi ya
kitunguu saumu kama tiba na kipodozi, ni jambo linalopendekezwa na wataalamu wa
urembo wa asili.
Katika matumizi yake kitunguu saumu
hutumika kwa kula na wakati mwingine kupaka, ambapo hili hutegemea zaidi na
mahitaji au matatizo ya mtumiaji husika.
Pamoja na njia hizo nilizotaja hapo
juu, lakini wataalamu wanashauri ulaji wa kitunguu saumu kibichi kila siku,
kwani husaidia kuboresha afya ya muhusika.
Ikiwa utashindwa kukitafuna chenyewe,
unaweza kuchanganya kwenye chakula kingine ambacho unatumia alimradi tu ukipate
kikiwa halisi.
Kwenye urembo, kitunguu saumu
husaidia kuondoa matatizo yafuatayo;
Chunusi
Changanya kitunguu saumu kilichosagwa
kijiko kimoja na kijiko kimoja cha juisi ya ndimu. Chukua pamba na paka sehemu
zote zilizoathirika. Kaa na mchangyiko huo kwa muda wa dakika 15 hadi nusu
saa.Ikiwa utaendelea kwa muda wa wiki moja. Tatizo la chunusi litakuwa
limeondoka kabisa.
Kunyonyoka kwa nywele
Ni kwa muda mrefu sasa kitunguu saumu
kimekuwa kikitumika kama tiba ya kunyonyoka kwa nywele. Unachotakiwa kufanya ni
kutumia mafuta yake kwa kupakaa kwenye ngozi ya kichwa kila siku kabla ya
kulala.
Fanya hivyo mara kwa mara kwa muda
usiopungua miezi mitatu na utaona matokeo yake. Ikiwa utakosa mafuta yake, si
vibaya ikiwa utatumia kitunguu chenyewe kilichosagwa kwa kupaka kwenye ngozi ya
kichwa kila siku usiku na kuosha asubuhi yake.
Fangasi vidoleni
Kupambana na fangasi kwenye vidole
vya miguu na mikono, unashauriwa kutumia kitunguu saumu kilichosagwa kwa kupaka
eneo lililoathirika. Hakikisha unakaa nacho usiku kucha ukiwa umevaa soksi ama
glavu. Fanya hivyo kila siku hadi utakapoona muwasho na maumivu yameisha.
MBA
Paka kitunguu saumu kilichosagwa
katika ngozi ya kichwa ama sehemu yeyote iliyoathirika. Hakikisha unatumia hadi
pale ugonjwa utakapokuwa umetoweka kabisa.
MATUMIZI KATIKA NCHIMBALIMBALI:
kitunguu ni kiambatanisho muhimu
kidishi kimaendeleo katika sehemu nyingi ulimwenguni.
Zamani Egpta iliheshimiwa kuwa ya
hadhi ya kimungu.
MAANDALIZI YA KITUNGUU SAUMU
KIMADAWA:
Kitunguu saumu na asali. Jaza chupa
ya glasi na vitunguu saumu vilivyomenywa na
kukatwa katwa polepole mwaga katika
asali ya kwamba inajaza nyufa katikati ya fundo ya
kitunguu. Weka glasi kwenye sehemu ya
joto yenye c 20oc. Katika siku mbili hadi wiki nne,
asali itanyonya juisi ya kitunguu
saumu na kitunguu hicho kitachechemea na kutoingiza
mwanga usichuje. Tumia katika muda wa
miezi 3.
Kitunguu Saumu dawa ya kikohozi
Ponda kijiko cha chai cha kitunguu
saumu katika kipimo hicho hicho cha sukari au asali.
Tumia mara moja k.mf. kwa kikohozi.
Kitunguu saumu mafuta. Weka g 200 za
vitunguu vilivyokobolewa saga kitunguu saumu na
kuweka kwenye chombo cha glasi na
ongeza mafuta ya kutosha (au vizuri mafuta ya chakula)
funga. Funga jagi kwa kubana vizuri,
na weka ikae kwenye sehemu yenye joto kama C 20
kwa siku tatu. Tikisa mara chache
kila siku. Halafu weka kwenye sehemu ya baridi, bila
kuchuja. Tumia katika muda wa mwezi
mmoja.
Kitunguu saumu „tinkcha“. Loweka g
200 za vitunguu vilivyomenywa na kukatwakatwa
katika lita moja ya brandi au
alikoholi 40-50%, kwa siku 14 kwenye C 20° katika chupa
yenye kufungwa vizuri bila kupitisha
hewa. Tikisa chupa hiyo mara nyingi kwa siku. Chuja
vipande vya kitunguu saumu. Tinkcha
inakaa muda wa mwaka.
MAPENDEKEZO YA MATUMIZI
Kula kitunguu saumu kibichi- hii ni
bora.
Tumia katika kupika.
Kula vitunguu saumu vingi kuzuia
magonjwa. Kitunguu saumu ni safi sana kwa mfano kuna
usemi kwamba, chakula chako kiwe
ndiyo dawa yako, na dawa yako chakula chako. Hii ni
kweli tu, hata hivyo, kwa kitunguu
saumu kibichi, kama ilivyo vitu vingi vyenye nguvu
vinaangamizwa katika kupikwa.
Vitunguu saumu vibichi vinatia nguvu katika mfumo wa
kinga ya maradhi. Matumizi kawaida ya
vitunguu saumu yameonyeshwa katika kupunguza
madhara ya magonjwa ya moyo,
kiharusi, kansa, msukumo wa damu na homa ya mafua
Makali (flu).
Tunashauri kwa nguvu ya kuwa
wanaoteseka kwa UKIMWI (AIDS) waweke
kitunguu saumu katika chakula chao
cha kila siku, kupunguza nguvu ya magonjwa mengine.
Kwa sababu inafanya mara mbili, kwa
matumizi ya nje na kwa ndani kama dawa ya kuua
wadudu, vitunguu saumu ni masaada wa
kutibu magonjwa yote ya kuambukiza; Toifodi,
minyoo, bilhazia, malaria, damu yenye
maambukizo na sumu n.k. Zaidi yake vitunguu saumu
vinaimarisha kumbukumbu, hupunguza
shindikizo la damu na Homa, na vinafanya kazi
kupinga ugumu wa kuta za ateri
(hardening of arteries). Vitunguu saumu pia vinapinga virusi
na dhidi ya kinyume cha mambo ya
fangasi.
1.Majipu au uvimbe na chunjua.
Saga vitunguu saumu vibichi na funga
vilivyopondwa kwenye sehemu ya jipu, uvimbe au
Chunjua mara mbili kwa siku na
gandamiza. Anza matibabu haya mapema iwezekanavyo.
2. Amiba.
Katakata vitunguu saumu sawasawa
vipande vidogo na chukua kijiko kikubwa 1 pamoja na
Chai mara tatu kwa siku (usitafune,
kusaidia kupinga kutoa harufu mdomoni). Endelea na
Matibabu haya kwa siku 5. I (H-M
Hirt) aliponywa mwenyewe toka Amiba kuharisha
damu kwa Tiba hii.
3. Malaria.
Katakata vitunguu saumu sawasawa.
Meza kijiko kimoja cha vitunguu hivi mara tatu kwa
Siku na kunywa lita 2 za limao glasi
ya chai kwa siku. Endelea na tiba hii kwa siku 5.
Angalia pia ukurasa wa 8 kwa ajili ya
malaria.
4. Kisukari, shindikizo la damu
kinga ya ugumu wa kuta za arteri
(hardening of the
arteries).
Kula vitunguu saumu kwa wingi,
vitunguu saumu na vitunguu vinapunguza sukari katika
damu na kusawazisha damu ya
cholesteroli, na shindikizo la damu. Badala yake chukua
matone 20 ya vitunguu tinkcha mara 3
kwa siku, basi hii ni pungufu ifuatayo:
5. Kikohozi, homa, sinusitis na
kuvimba koo.
a) Kula klovu ya vitunguu saumu mara
tatu kwa siku.
b) Chukua kijiko cha chai cha
kitunguu saumu asali kila masaa machache.
c) Watoto wanaweza kutumia kijiko cha
chai cha kitunguu saumu
mchanganyiko kila baada ya masaa
machache.
d) Chukua kijiko cha chai cha
kitunguu saumu mafuta mara 6 kwa siku.
6. Kandika.
Chukua kijiko cha chai cha kitunguu
saumu au kitunguu saumu yenye asali, kila masaa
machache. Weka mdomoni kwa muda mrefu
iwezekanavyo.
7. Fangasi inayoambukiza pamoja na
ugonjwa wa ukungu kwenye vidole vya miguu.
Funga sehemu zilizoathirika kwa juisi
ya vitunguu saumu vibichi vilivyopondwa au
mafuta.
8. Homa ya matumbo na maambukizo
mengine.
Kama itatokea homa ya matumbo,
bacillary, kuharisha damu, kifua kikuu, kipindupindu,
trypanosomiasis (ugonjwa wa
kusinzia): Siku zote ongeza kitunguu saumu kwa tiba ya
kawaida.
9. Kinga ya mishipa ya damu.
Kitunguu saumu siku zote kinafanya
damu kuwa laini na kukinga kutengeneza damu
kuganda ambayo inasababisha shida ya
thrombosis. Hii ni muhimu kwa wagonjwa wanaolala kitandani kwa muda mrefu.
10. Kuota meno utotoni.
Futa ufizi kwa fundo la kitunguu
Saumu.
Kitunguu thaum kina harufu ya pekee
isiyowapendeza watu wengi, ingawa kimebeba siri nyingi za tiba. Kwa ajili hiyo
maanayake kwa kilatini ni : harufu ichomayo, na kwa kiarabu lugha ya Quraan
huitwa: fuum, nayo ndio sahihi zaidi; kwasababu thaum ni lafdhi ya kihieroglifu
ya kifirauni (hieroglyphic).
Allah S.W amesema:
" Na (kumbukeni habari hii
kadhalika) Mliposea: Ewe Mussa! hatuwezi kusubiri chakula cha namna moja tu,
basi tuombee kwa Mola wako atutolee vile vinavyooteshwa na ardhi kama mboga
zake, matango yake, fuum (kitunguu thaum) zake, adesi zake na vitunguu
vyake." (2:61)
Iliandikwa katika piramidi (pyramid)
huko Misri tangu miaka 4500 iliopita kuwa kitunguu thaum kilikuwa wakipewa
wajenzi ya piramidi. Walikuwa wakila kitunguu thaum ili wapate nguvu na
nishati.
Mwandishi wa kitabu juu ya tiba
zinazotokana na kitunguu thaum alimnasihi mfasiri wake kuwa " Iwapo
unataka nguvu, nishati na uwekevu basi kula tembe ya kitunguu thaum na glasi ya
maji kila siku kabla ya kula chakula. Daud Al-Antaky ameeleza katika kitabu
chake cha Tadhkira kuwa kitunguu thaum hupoza zaidi ya maradhi 40.
Wale wapiganaji wa miereka wa huko
Roma walikuwa wakila kitunguu thaum kabla ya kupigana ili wapate nguvu na
wepesi.
Imethibitishwa kisayansi kuwa
kitunguu thaum husafisha damu kutokana na mafuta (cholestrol) ambayo
husababisha magonjwa ya mishipa ya ateri na maradhi ya moyo, na pia husafisha
damu kutokana na vijidudu na maikrobati kuliko (antibiotic) vengine. Pia
imethibitishwa kwa kuzuia kuenea kwa sumu ya nyoka katika mwili wa mwanaadam na
pia husafisha maida kutokana na vimelea (parasites).
Rais wa matabibu, Ibn Sina amesema
kuhusu kitunguu thaum: "Kitunguu thaum hulainisha na kuondoa gesi, hutoa
vidonda katika ngozi, huhifadhi maji. Vumbi lake likichanganywa na asli
akipakwa mwenye ukoma litamfaa, kitunguu thaum humfaa mwenye maradhi magonjwa
ya mishipa na nyonga (sciatia). Maji yake (yaliotolewa kwa kupikwa) hutuliza
maumivu ya meno, vilevile hufaa kwa kikohozi.
Kitunguu thaum kimekusanya protein
49% mafuta muhimu ya sulphur 25% na kiasi flani cha chumvi, homoni (hormones)
zitiazo nguvu za kiume na vinavyoteremsha hedhi.
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA
KITUNGUU SAUMU:
Kiua Sumu:
Saga tembe tano za kitunguu thaum,
changanya na asali kikombe kimoja kilichochanganywa na habbasouda na kunywa
papo hapo. Kunywa asubuhi na jioni. Paka mafuta ya kitunguu thaum pahala
panapouma iwapo ni sumu ya nyoka au paka nje ya tumbo iwapo umekunywa sumu.
Kusafisha tumbo:
Kabla ya kula chakula, meza tembe za
kitunguu thaum na baadae kunywa maji ya shimari yaliyochanganywa na asali kwa
muda wa wiki moja.
Kiyeyusha mafuta (Cholestrol):
Unapokula chakula kila siku, weka
katika kachumbari kiasi cha tembe 2 vilivyosagwa ule pamoja na kachumbari.
Kiongeza mkojo chenye kusafisha njia
za mkojo:
Chemsha vizuri hairi, na baada ya
kupoa tia tembe 3 za kitunguu thaum zilizosagwa. Kunywa kinywaji hicho kila
siku kabla ya kula na kunywa juisi ya limau/ndimu.
Kuharisha damu (Dysentery):
Chukua tembe ya kitunguu thaum
uikatekate na uile; fanya hivyo kwa muda wa wiki moja na bora zaidi ukinywa na
mafuta ya zaituni kijiko kimoja.
Gesi na Indegestion:
Kunywa juisi ya pea iliyochanganywa
na tembe 3 za kitunguu thaum kabla ya kulala kila siku.
Kutibu Typhoid:
Kata tembe 5 za kitunguu thaum,
changanya ndani ya maziwa ya moto yaliyochanganywa na asali kunywa kabla ya
kulala. Pia paka uti wa mgongo mafuta ya kitunguu thaum yaliyochanganywa na
mafuta ya zeti, na asubuhi vuta moshi wa kitunguu thaum kwa muda wa dakika 5.
Kidonda kilichooza:
Ponda kitunguu thaum mpaka iwe laini
kama marhamu halafu jifunge nacho kwa kutumia bendeji, japo kitawasha lakini
kitazuia ugonjwa wa gangrene ambao unaweza ukapelekesha kukatwa kiungo.
Vilevile unaweza kusafisha kidonda kwa kuchanganya kitunguu thaum kilichosagwa
kikatiwa maji vuguvugu (warm water) na kikasafishwa kidonda.
Mishipa:
Kata tembe za kitunguu kitunguu saumu
na umeza kwa maziwa ya moto (sio moto sana) yenye matone ya ambari kabla ya
kulala kila siku, dawa hii huipa mishipa nguvu.
Homa ya mafua (Influenza):
Kunywa juisi ya machungwa na juisi ya
limau zilizochanganywa na tembe 7 za kitunguu thaum kunywa juisi hiyo kabla ya
kulala. Vuta moshi wa kitnguu thaum.
Mafua:
Meza tembe za kitunguu thaum baada ya
chakula pamoja na juisi ya kitunguu thaum iliyochanganywa na juisi ya limau
pamoja na kuvuta moshi wa kitunguu thaum.
Saratani (Cancer):
Katika kitunguu thaum kuna kiini
kinachozuia saratani, kwa kila mgonjwa wa saratani anashauriwa ale kwa wingi
kitunguu thaum na karoti (carrot).
Kifua kikuu (cha mapafu):
Kila asubuhi kabla ya kula chakula
meza tembe 3 za kitunguu thaum, saga ule pamoja na mkate na jioni vuta moshi
wake.
Kipindupindu (cholera):
Ili kujikinga na maradhi hayo wakati
kikienea, kula kijiko kimoja cha kitunguu thaum kilichosagwa na kukorogewa
katika asali baada ya kila chakula.
Kutoa minyoo:
Ponda tembe 3 za kitunguu thaum, tia
ndnai ya maziwa na kunywa (bila kutia sukari) jioni kabla ya kulala na asubuhi
kunywa mafuta ya mbono.
Upele:
Chukua tembe 5 za vitunguu thaum
uvisage na uvikoroge katika shahamu na paka pale penye upele kuazia jioni mpaka
asubuhi na ukoshe kwa maji ya moto tumia kwa muda wa wiki moja.
Mbaa kichwani:
Ponda uzuri vitunguu thaum 3 na
uvikoroge katika siki ya tofaha (Apple vinegar) katika chupa ya bilauri (sio
plastiki) na uache juani kwa muda wa wili moja. Baada ya hapo jipake kichwani
pamoja na kusugua kwa muda wa wili 1 na baada ya wiki jipake mafuta ya zeituni.
Nguvu za kiume:
Saga kitunguu thaum kitie ndani ya
mafuta ya zeti na weka katika moto mdogo mdogo mpaka iwe rangi ya manjano na
tia katika chupa na wakati wa haja jipake katika dhakari na osha baada ya saa
moja.
Kujenga misuli na kutia nguvu:
Kila siku kabla ya kula kunywa
kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia yaliyotiwa tembe 2 za kitunguu thaum
iliyosagwa. Kunywa kwa muda wa mwezi mmoja mfululizo.
Kinga ya taunni na ukimwi:
Ngao kubwa ya maradhi mabaya ni
Kumcha Allah S.W mwanzo na mwisho wa siku. Chukua juisi ya kitunguu thaum
uichanganye na asali na unywe utafanya hivo pamoja.
KITUNGUU SAUMU.
tangu kale kimekuwa kikijulikana kama
'dawa ya kushangaza' na kutumiwa na watu wengi katika kutibu mafua na
influenza. Miongoni mwa faida za kitunguu swaumu ni kuzuia kupatwa na magonjwa
mbalimbali na maambukizo ya virusi. Hivyo kitunguu swaumu hujulikana kama
antibiotiki ya asilia. Uchunguzi umeonyesha kwamba kula kitunguu swaumu
kunapunguza kushadidi ugonjwa wa influenza na hata kuzuia kupatwa na ugonjwa
huo. Vilevile kula kila mara kitunguu swaumu, huzuia kupatwa na magonjwa ya
moyo, kwani kitunguu swaumu huzuia damu isigande kwenye mishipa ya damu.
Halikadhalika kitunguu swaumu ambacho
pia ni kiungo muhimu cha chakula kina potassium, na hivyo watu wenye ugonjwa wa
shinikizo la damu wanashauriwa kula vyakula vilivyopikwa kwa kitunguu swaumu.
Si vibaya kujua kuwa katika uchunguzi
uliochapishwa mwaka 2001, imeelezwa kwamba, kitunguu swaumu kina athari kubwa
na nzuri pale kinapochanganywa na baadhi ya dawa nyinginezo katika kutibu
Ukimwi au HIV.
Haya shime jamani… kuanzia leo
vyakula visikose kuungwa na kitunguu thomu, iwapo unaogopa kupatwa na influenza
kama mimi!
MADHARA YAKE:
Kitunguu saumu kinaweza kukera ngozi
hasa baada ya kutumia kwa muda mrefu. Epuka
kuhusisha kwenye macho.
No comments:
Post a Comment