Utafiri wa kiashirio cha VVU/UKIMWI na malaria Tanzania 2011-2012 umejumuisha kwa
kupima zaidi ya wanawake na wanaume20,811. Kwa mujibu wa utafiti huo asilimia 5.1 ya
watanzania wenye umri wa miaka 15-49 wanamaambukizo ya VVU/UKIMWI.
Maambukizo ya VVU/UKIMWI ni ya kiwango cha juu miongoni mwa wanawake kuliko
wanaume katika maeneo ya mijini na vijijini. Wakazi wa mijini ni mara mbili zaidi ya wakazi wa vijijini.
Maambukizo ya VVU/UKIMWI Tanzania yamepungua katika miaka ya hivi karibuni.
Kiwango cha hivi karibuni cha maambukizo ya VVU/UKIMWI ni 5.1% ambapo 6.2% ni wanawake na 3.8.% ni wanaume. Kwa kulinganisha na utafiti wa kiashirio cha VVU/UKIMWI Tanzania mwaka 2007-2008 (THIS) umebaini maambukizo ya jumla ya VVU/UKIMWI kuwa ni 5.7%,
Maambukizo ya VVU/UKIMWI ni ya juu zaidi katika mkoa wa Njombe (14.8%),
Kiwango cha maambukizo ni cha chini zaidi Pemba ambayo ni chini ya (1%).
Kwa wanawake na wanaume viwango vya maambukizo ni vya juu zaidi miongoni mwa
wajane au walio talikiwa (walioachwa) kuliko wajane au wasio oa au kuolewa au walio oana hivi karibuni. Kati ya wanawake wajane wanne, mmoja ana virusi.
Visababishi vya VVU/UKIMWI
Mwenendo na vibainishi vya janga la UKIMWI nchini ni vingi na vinaongozwa na
uhusiano wa kingono wa watu wa vipengele vingi vya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi. Kwa ujumla, vibainishi vya janga la UKIMWI nchini huenda visitofautiane sana na vile vya sehemu nyingine za Afrika zenye maambukizo ya UKIMWI
yaliyoenea nchi nzima. Miongoni mwa vipengele muhimu ni pamoja na vifuatavyo:
v
Uasherati
v
Matumizi madogo na yasiyo
endelevu ya kondomu
v
Ngono za marika
yanayotofautiana sana
v
Kuwa na wapenzi wengi.
v
Ukosefu wa elimu ya
maambukizo ya UKIMWI
v
Kuwepo kwa maradhi mengi
ya ngono kama vile tutuko, homa,
v
Jando kwa wanaume
Sababu za mahali husika, za kushamiri kwa janga nchini ni:
Ø
Umaskini na biashara ya
ngono pamoja na ongezeko la wafanyabiashara
wa ngono
Ø
Tabia mbaya za ngono za
wanaume kutokana na kuruhusiwa kimila kuwa
na nguvu
Ø
Kukosekana usawa wa
kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijinsia pamoja na
unyanyaswaji wa wanawake na
wasichana walio ndani na nje ya mahusiano.
Ø
Matumizi ya pombe na dawa
za kulevya.
Ø
Tabia za kimila (kama
vile utakasaji wajane na jando na unyago)
Ø
Safari za aina zote
zinazosababisha kuwa mbali kwa wanandoa
na ongezeko la mahawara
Ø
Kutokutahiriwa
|
Saturday, 29 November 2014
HALI YA SASA YA VVU/UKIMWI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment