Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambayo inafahamika na wengi katika jamii kutokana na ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo. Wapo wanaoitumia kama kiungo cha mboga na wengine huifanya mboga kamili. Bamia ina majina mengi, wengine huiita okra na kwa jina lisilo rasmi Kiingereza huitwa, 'lady finger' au gumbo. Bamia kwa kawaida hulimwa zaidi kwenye maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo maeneo makavu, na mboga hiyo imekuwa ikitumika kwa miaka mingi katika historia ya lishe na matibabu ya mwanadamu kutokana na faida zake nyingi kiafya.
Kama lilivyo tunda la kiwi, bamia inajulikana kwa kuwa na kiasi kingi cha vitamin C, vitamin K na folic acid. Pia bamia ni maarufu kwa kuwa na ufumwele mwingi unaosaidia tumbo kusaga chakula vizuri na kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Si hayo tu bali bamia ina vitamini A nyingi ambayo husaidia kutengeneza kinga ya sumu. Kwa kifupi, sumu inapoingia mwilini bamia huzuia kusambaa kwake. Vitamini A itokanayo na mboga hiyo husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na maradhi. Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara huimairisha mwanga katika macho yao. Wingi wa vitamini A huzuia maradhi yanayotokana na virusi kama vile mafua. Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Watu wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia kujenga ngozi. Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo. Kama tulivyosema vitamini K iliyopo kwenye mboga hiyo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.
Vitamini kadhaa zilizoko kwenye mboga ya bamia kwa ujumla tunaweza kusema inasaidia katika magonjwa mbalimbali. Uchunguzi umeonesha kuwa, kula bamia husaidia katika magonjwa ya figo. Katika uchunguzi huo imeonekana kuwa wale ambao wanapendelea kula bamia, mboga hiyo inaweza kuwakinga na ugonjwa wa figo. Kutokana na ufumwele mwingi iliyokuwa nao pia bamia huimarisha afya ya utumbo kwa kusaidia kusafisha mfumo wa kusaga chakula. Taban faida za bamia ni nyingi lakini tutakazozitaja hapa ni kuzuia kisukari, kusaidia katika ujauzito, kuondoa mada hatari mwilini zinazoweza kusababisha saratani na pia kuponya magonjwa kama asthma, kukohoa na matatizo ya kupumua.
#######################################################
Kabichi ni mboga ya majani ambayo licha ya kulimwa kwa wingi na kupatikana masokoni karibu katika kipindi chote cha mwaka lakini wapishi wengi huwa hawaitumii sana katika milo. Hata hivyo kama unataka kuwa na ngozi inayong'aa na mfumo wa kinga ya mwili ulioimarika ili kupambana na maradhi ya aina yoyote pengine unapaswa kutoishia tu kutumia kabichi kwenye saladi na kachumbari na kuanza kula mara kwa mara mboga hiyo. Hii ni kwa sababu, kabichi ni mboga yenye nguvu hali iliyowapelekea waganga wa jadi kusema kuwa kabichi ina nishati inayotokana na mwezi kwa kuwa inakua katika mwanga wa mwezi. Hata kama hatutoamini ngano hizo lakini wataalamu wa sasa wa lishe wanasema kuwa, nishati inayopatikana kwenye kabichi inatokana na kiwango kikubwa cha sulphur na vitamin C na kwa ajili hiyo si vibaya ukizingatia chakula hicho katika mlo wako. Miongoni mwa faida za kabichi ni kusaidia katika kupunguza unene, na sifa hiyo inatokana na kalori ndogo ilizonazo na ufumwele wingi. Kikombe kimoja cha kabichi kina kalori 33 tu, hivyo ni chakula kinachofaa kwa ajili ya kupunguza unene. Kabichi pia huongeza akili, na hii ni kutokana na kuwa na vitamini K na mada ya anthocynins inayosaidia ubongo kufanya kazi vizuri na kuzingatia mambo. Virutubsho hivyo pia huzuia neva kuharibika, kuimarisha siha dhidi ya ugonjwa wa kusahau na Alzheimers. Kabichi yenye rangi nyekundu ina virutubisho hivyo kwa wingi. Ingawa mboga zote zina faida kwa ngozi, lakini kabichi inaongoza! Kutokana na kuwa na sulfur, kabichi husaidia kukausha ngozi yenye mafuta na chunusi. Ndani ya mwili pia sulfur ni muhimu kwa ajili ya kutengeneza keratin, protini ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya nywele, kucha na ngozi.
##########################################################
Miongoni mwa faida nyingi zinazopatikana kwa kula kabichi (nyeupe na nyekundu), inayoongoza ni kuukinga mwili na ugonjwa hatari wa saratani. Inaelezwa kuwa, zaidi ya tafiti 475 zimefanyika kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye kabichi na kuthibitisha kwamba, vina uwezo wa kuzuia ugonjwa wa saratani na wakati mwingine hata kutibu. Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee wa kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za mada za 'Antioxidant', 'Anti-inflammatory' na 'Glucosinolates,' ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababisha saratani za aina mbalimbali mwilini. Kwa kuzingatia madhara na mateso yatokanayo na ugonjwa wa saratani, na kwa kuzingatia upatikanaji wa kabichi usiokuwa na gharama, huna sababu ya kupuuza ulaji wake. Laiti kama watu wote tungejua sawasawa faida za kabichi, bila shaka mboga hii ingekuwa ghali kuliko hata samaki.
Wapenzi wasikilizaji faida za kabichi haziishii hapo, kwani mboga hiyo ina kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin hasa vitamini K, B1, B2, vitamin A na C. Aidha, kabichi ina kiasi kingi cha ufumwele au kamba lishe kwa maana ya fiber kwa kimombo, manganizi, potashiamu na fatty acids. Vyote hivyo ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi. Mbali na kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani, juisi ya kabichi
inaelezwa kuwa na faida nyingi tumboni, hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo (peptic ulcers). Ikitumika mara kwa mara huwa kama tiba kwao, na mfumo wa usagaji chakula tumboni, huwa imara.
###################################################
Na tunahitimisha kipindi chetu kwa kuelezea faida za brokoli kiafya. Mboga hii ni mingoni mwa vyakula vilivyopata umaarufu katika siku za hivi karibuni, kutokana na faida zake kiafya. Hii ni kwa sababu unapokula mboga unaupatia mwili wako virutubisho vingi na pia jinsi mboga hiyo inavyoweza kuliwa pambozini mwa vyakula vingine huku ikiwa na kalori chache. Brokoli inafanana na cornflower isipokuwa ina rangi ya kijani na ni mboga yenye virutubisho vingi kama vitamin K, A, C, ufumwele, potassium, Folic Acid na lutein. Miongoni ma faida za mboga hiyo ni kusaidia mfumo mzima wa neva na ubongo kufanya kazi inavyotakiwa na pia kuipatia nguvu misuli. Brokoli inasadia pia msukumo wa damu kuwa sawa, inapambana na sumu mwilini na kusaidia na kujenga mifupa. Pia zink na seleniam zilizoko kwenye brokoli husaidia kuifanya kinga ya mwili kuwa imara.
Faida nyingine ya mboga ya brokoli ni kupunguza allergy na uvimbe mwilini. Na sifa hiyo inatokana na kuwa na mada za kaempferol na isothiocyanates ambazo zote huzuia uvimbe na kuondoa maumivu. Pia Brokoli ina omega 3 ambayo ni maarufu kwa kuondoa maumivu. Pia kula mboga hii husaidia chakula kusagwa vyema, kuzuia kukosa choo, kushusha sukari kwenye damu na kuzuia kula kupita kiasi. Kikombe kimoja cha brokoli kina protini sawa na kikombe cha wali au mahindi lakini kiwango chake cha kalori ni nusu. Pia brokoli kama zilivyo mboga nyinginezo huufanya mwili usiwe na acidi, suala ambalo lina faida nyingi kiafya. Kuhusiana na saratani mboga hii haikuachwa nyuma, kwani brokoli ina glucoraphanin ambayo hubadilishwa mwilini na kuwa sulforaphane mada inayozuia kensa. Mada hiyo huua bakreria aina ya H. Pylory ambao huweza kusababisha kensa ya utumbo. Naam wapenzi wasikilizaji, baada ya kufahamu faida za mboga hizi ni matumaini yetu kuwa hazitokosekana katika milo yetu, daima tuzitunze afya zetu!
No comments:
Post a Comment